Billboard Yatoa Orodha Ya Wasanii Bora Wa Karne 21, Mashabiki Wapinga

Billboard Yatoa Orodha Ya Wasanii Bora Wa Karne 21, Mashabiki Wapinga

Chati kubwa ya muziki Duniani ya Billboard imetoa orodha ya wasanii 100 bora na waliofanya vizuri kwenye chati hiyo kwa karne ya 21, kuanzia miaka ya 2000 mpaka 2024.

Chati hiyo ambayo imeongozwa na mwanamuziki Tylor Swift akiwa namba moja akifuatiwa na Drake (2), Rihanna(3), Post Malone(4), na Eminem(5) ambao wameshika nafasi 5 za juu imepingwa na baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Billboard kwenye upande wa komenti mashabiki wameonesha kupinga orodha hiyo wakidai kuwa haiko sawa huku wengi wao wakipinga Chris Brown kuwekwa nafasi ya 18 kwani anastahili kuwa Top 10 ya chart hiyo.

Mbali na hilo lakini pia mashabiki walionesha kuchukizwa zaidi na orodha hiyo kuondoa kundi la BTS kutokana na kundi hilo kuwa ni miongoni mwa makundi yanayofanya vizuri katika kiwanda hicho cha burudani.

Aidha Billboard iliweka wazi kuwa nafasi hizo za wasanii zimetokana na uingizaji wao wa Albumu kwenye hot 200 za kila wiki kwenye chati hiyo na chati ya nyimbo 100 za Billboard Hot 100 kuanzia mwanzo wa mwaka 2000 hadi mwisho wa 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags