Baba Levo Akubali Kipaji Cha Rose Ndauka

Baba Levo Akubali Kipaji Cha Rose Ndauka

Mwananmuziki na mtangazaji Baba Levo amekikubali kipaji cha msanii na mwigizaji Rose Ndauka huku akimtabiria kufika mbali zaidi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Baba Levo amempongeza msanii huyo huku akimtaka kuongeza bidi ili kuwafunga midomo baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki wanaodai kuwa msanii huyo hajui kuimba.

“Kama kuna watu Wanamdharau Rose Ndauka kwenye muziki basi watapata aibu huko mbeleni mimi naona ana kipaji kikubwa sana anatamba na beat vizuri mno. Keep going mimi naona unavyoenda kuwashangaza soon,” ameandika Baba Levo

Aidha kupitia posti hiyo upande wa komenti Ndauka alitoa shukrani kwa Baba Levo kufuatia na kitendo cha kukubali kipaji chake. “Hii ni kubwa sana kwangu, ahsante sana kaka mkubwa one,” ameandika Ndauka

Baba Levo sio msanii wa kwanza kuukubali kipaji cha Ndauka, naye mwanamuziki Frida Amani alionesha kuvutiwa na ngoma za mwanadada huyo huku akiwataka mashabiki kusikiliza ngoma kwa makini na kuacha kuzikiliza kwa vibe.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags