Kheri ya mwaka mpya!
Ni mwanzo wa mwaka 2025, walioajiriwa na wafanyakazi wa sehemu mbalimbali wanarudi kazini baada ya mapumziko ya sikuku za mwisho wa mwaka. Zingatia mambo haya unaporudi kazini ili kuongeza ufanisi na imani kwa watu unaofanya nao kazi.
Fanya kazi yako vizuri
Hili la kwanza linaweza kuwa wazi. Umeajiriwa kwa sababu mwajiri wako anahitaji msaada kutokana na ujuzi ulionao. Unategemewa kufanya kazi zako kwa juhudi na maarifa.
Zingatia maelekezo sera na kila kitu kinachohusiana na kazi yako, timiza wajibu wako kama kazi yako inakwenda sambamba na vitu kama “deadlines” hakikisha unafanikiwa ipasavyo katika hilo.
Malengo
Nimuhimu kuwa na malengo yako binafsi kama mfanyakazi ukiachana na malengo ya ofisi ili kuongeza ufanisi wako kazini jiwekee malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu yasimamie ili utatimize lakini hakikisha malengo yako hayaathiri malengo ya ofisi ili usije tofautiana na kazini kwako weka malengo ya kuwa bora bila kuathiri mifumo ya ofisini kwako.
Ongeza ushirikiano na wafanyakazi wenzako
Shirikiana na wafanyakazi wenzako kwa kiasi kikubwa washirikishe kile ambacho unaona kitakuwa na manufaa kwenye ofisi yenu lakini pia usisite kutoa mchango wako pale ambapo unaona unaweza kuchangia mawazo kwenye suala fulani ofisini wape mawazo yenye madini na yenye kuijenga ofisi yenu.
Endelea kujifunza
Kama unafanya kazi kitengo ambacho kinahitaji mtu kujiboresha zaidi kwenye masuala mbalimbali kwa njia ya kujifunza usiogope kujifunza, angalia namna gani wenzako waliokutangulia au waliowazidi ofisi kwenu wao wanafanyaje kazi jifunze kisha boresha zaidi ilikuwa sambamba na mahitaji ya sasa.
Kuwa mwaminifu
Bila shaka hili linajieleza, uaminifu katika kazi na maishani kwa ujumla ni silaha nzuri katika mambo mengi.
Bado nakumbuka jinsi Rais mstaafu Hayati Benjamin Mkapa alivyowaasa vijana katika suala zima la kuwa waaminifu ili kwenda sambamba na changamoto za maendeleo ya kiuchumi.
Leave a Reply