Mfahamu Miss Ukraine aliyepambana na Urusi

Mfahamu Miss Ukraine aliyepambana na Urusi

Peter Akaro

Miss Ukraine mwaka 2015, Anastasia Lenna mnamo Machi 2022 aligonga vichwa vya habari ulimwengu mara baada ya kuweka wazi ataingia vitani kuisaidia nchi yake dhidi ya uvamizi wa Urusi kwa kile kinachoitwa operesheni maalumu ya kijeshi.

Hata hivyo, tangazo la Anastasia kama raia wa kawaida na mtu maarufu upande wa urembo na mitindo, lilivuta hisia za wengi ambao wamekuwa wakisambaza picha alizovalia kijeshi mtandaoni. Je, huyu ni nani hasa?.

Anastasia Lenna anajulikana sana kwa kazi yake kama Mwanamitindo kitaaluma, huyu ni malkia wa urembo wa zamani ambaye alishindana katika shindano la urembo la Miss Grand International la 2015 na kuibuka mshindi.

Anastasia aliyezaliwa mwaka 1998, kwa sasa Mwigizaji, kazi aliyoipenda tangu akiwa na umri wa miaka 13, huku akitajwa kuwa na uwezo wa kuzungumza lugha tano.

"Kila nilipoenda nilifanya chochote ili kupata nafasi ya kuingiza na kupiga picha. Mungu alinipa mrembo huu kwa sababu fulani," anasema Anastasia kupitia tovuti yake.

Ukiachana na Mitindo na Uingizaji, Anastasia ni Mtangazaji wa Televisheni akiwa na kipindi chake cha muziki kiitwacho "World Top 10" kinachoruka kwenye chaneli ya Kituruki, Genc TV.

Huyu ni msomi wa Shahada (Degree) toka Chuo Kikuu cha Slavistik cha Kyiv, akisomea Usimamizi wa Masoko, baada ya kuhitimu alienda Uturuki na kufanya kazi kwenye miji kama Istanbul, Ankara na Bodrum kama Meneja wa Mahusiano kwa Umma.

Utajiri wake unakadiriwa kufikia Dola2 milioni ambazo ni sawa na wastani wa Sh4.2 bilioni. Ana wafuasi zaidi ya 300,000 kwenye mtandao wa Instagram ambao ndio aliutumia kutangaza hatua hiyo na amekuwa akiutumia kuikemea Russia. Aliwahi kuandika kuwa;

"Mimi si Mwanajeshi, ni mwanamke tu, ni binadamu wa kawaida tu. Mtu tu, kama watu wote wa nchi yangu, sifanyi propaganda yoyote isipokuwa kuonyesha kuwa ni mwanamke wa Ukraine, hodari, anayejiamini na mwenye nguvu".



"Ninashukuru umakini na msaada kwa nchi yangu, watu wote nchini Ukraine tunapigana kila siku dhidi ya uchokozi wa Urusi.Tutashinda!,"

"Watu wa Ukraine hawana hatia, hakuna kati yetu aliye na hatia yoyote, tuko kwenye ardhi yetu! Ninazungumza na watu wote wa Ulimwengu!, acheni vita nchini Ukraine! hakuna watu wanapaswa kufa!" alisema Anastasia Lenna.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags