Msanii Chemical atunukiwa Shahada ya Uzamivu PhD nchini Uingereza

Msanii Chemical atunukiwa Shahada ya Uzamivu PhD nchini Uingereza

Msanii wa hiphop nchini, Chemical ambaye alikuwa masomoni Uingereza amefaulu mtihani wa mahojiano wa PhD (Viva Voce) wa shahada ya Uzamivu (PhD) katika chuo cha St. Andrews nchini humo.

Chemical amesema kufikia hatua hiyo ya elimu ilikuwa ndoto yake ambayo kwa sasa imetimia.

"Niliwahi kuwa na ndoto na leo nimeamka kama Dk Lubao. Nina shauku zaidi ya kushiriki kwamba nimepitisha rasmi PhD Viva yangu, ninaheshimu na kushukuru sana kwa usaidizi wa ajabu ambao nimepata kutoka kwa wasimamizi wangu, idara shirikishi, kamati ya ukaguzi, wasahihishaji, washiriki.

"Wafanyakazi wenzangu, marafiki, muziki na familia yangu, na kila mtu ambaye alinitia moyo katika safari hii yote ya kuwa Dk. Lubao.
Usiku usio na usingizi, kujitolea, uvumilivu yote yamelipa," ameeleza Chemical.

Utakumbuka, Chemical aliwahi kutunukiwa tuzo kutoka University Of Dar es Salaam mwaka 2021, kwa kuwa mwanafunzi mwenye tafiti bora zaidi 2020/2021 ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika;

"Nimekua mwanafunzi mwenye tafiti bora (first winner) kwa chuo kizima kwa mwaka 2020/21. Chuo cha UDSM ni kikubwa wanafunzi ni wengi na wanafanya vitu vikubwa sana.Mimi kushinda nafasi hii ilikua ni ndoto ambayo sikuwahi kuiota.

"Lakini namshukuru mwalimu wangu Dr. Elgidius Ichumbaki kwa kusimamia taaluma yangu, kuni-train mpaka leo niliyohisi hayawezekani yamewezekana thank you team for mentoring me. Niseme tu kwamba miaka miwili niliyotulia kwenye muziki haikwenda bure," aliandika Chemical.

Chemical amewahi kutamba na nyimbo kama I'm sorry mama,You and I, New Material, Kemikali na nyinginezo. Baada ya msanii huyo kuonesha furaha yake ya kufikia kiwango hicho cha elimu. Mashabiki wake kutoka sehemu mbalimbali wamempongeza kupitia uwanja wa komenti.

Mwanamuziki Frida Aman amempongeza kwa kuandika "Dr Lubao🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 congratulations lakini". Aidha Mummy Baby ameandika "Dr Lubao i am very very proud of you 'guu bavu' Mungu azidi kukuongoza".

Pia, Osmund Mbangati ameandika "Hongera sana kwa kufaulu PhD yako Viva! Hiyo ni habari ya nzuri. Haya ni mafanikio makubwa Dr. Lubao, najua ni kwa kiasi gani ulifanya bidii kwenye PhD yako, na ni ya muhimu kwa watu hasa kutoka Tanzania. PhD imehakikishwa na umefanya vizuri tena Dk. Lubao"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags