Wayne, Drake, Nicki Minaj Mtaji Tosha Kwa Birdman

Wayne, Drake, Nicki Minaj Mtaji Tosha Kwa Birdman

Rapa nguli wa Marekani na mmiliki wa lebo ya muziki ya Cash Money Records, Birdman amesema alipata mafanikio makubwa kupitia wasanii Lil Wayne, Drake, na Nicki Minaj.

Birdman ameyasema hayo kwenye mahojiano na Podcast ya NickCannon iitwayo Cannon's Class akisema hadi sasa wasanii hao wamemuingizia zaidi ya dola bilioni 2.

“Drake, Nicki, na Wayne wamenipa mzigo wa kutosha, si chini ya dola 2 bilioni,”amesema Birdman.

Hata hivyo, hiyo sio mara ya kwanza kwa Birdman kujigamba kuhusu pesa anayopata kupitia wasanii hao watatu. Utakumbuka 2021 alipokuwa kwenye mahojiano na Big Fact Podcast alidai aliwapa wasanii hao dola 1.4 bilioni baada ya kusaini mkataba mkubwa na kampuni ya Universal Music.

“Universal waliponipa mzigo mzito, naweza kusema kwa uaminifu nilimpa Wayne kati ya dola 400 milioni hadi 500, Drake alipata karibu dola 500 milioni, na Nicki alipata kati ya dola 300 hadi 400 milioni kutoka mfukoni mwangu,” alisema Birdman.

Hata hivyo Drake na Lil Wayne waliondoka rasmi kwenye lebo ya Cash Money mwaka 2018 Wayne akienda kuendeleza lebo yake ya Young Money aliyoinzisha tangu mwaka 2005.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags