Jux Afanywa Mfano Nigeria

Jux Afanywa Mfano Nigeria

Mfanyabiashara wa Nigeria na rafiki wa mke wa msanii wa Bongo Fleva Jux, Chioma amewashauri wasanii nchini humo, kuweka juhudi katika utumbuizaja wanapokuwa jukwaani.

Chioma ametoa ushauri huo akitolea mfano shoo ya Jux aliyofanya kwenye ugawaji wa Tuzo za Headies zilizofanyika usiku wa jumapili Lagos Nigeria.

''Natamani wasanii wa Nigeria wangeanza kuweka juhudi zaidi katika maonyesho yao kama Juma alivyofanya," amesema Chioma.

Ameongezea kuwa utumbuizaji mwingi wa wasanii wa Nigeria ni wakivivu na hawafanya mazoezi kabla ya shoo.

Hata hivyo, Chioma amesema watu wasimnukuu vibaya kwani sio wasanii wote wa Nigeria hawajui kupafomu wapo ambao ni wazuri zaidi kwenye majukwaa.

"Msininukuu vibaya sio wasanii wote hawajui, wapo ambao ni wazuri jukwaani," amesema.

Sifa hizo kwa msanii wa Bongo Fleva Juma Jux zimetolewa baada ya kufanya pafomansi kali kwenye ugawaji wa tuzo za The Headies zilizofanyika weekend iliyopita Lagos, Nigeria






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags