Aliishi Kwenye Dali La Ex Wake Kwa Miaka 12

Aliishi Kwenye Dali La Ex Wake Kwa Miaka 12

Katika tukio la kushangaza lililotokea Rock Hill, South Carolina mwaka 2012, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Tracy aligundua kuwa mpenzi wake wa zamani (EX) alikuwa akiishi kwa siri kwenye dali ya nyumba yake kwa kipindi cha miaka 12 baada ya kuachana.

Inaelezwa kuwa mwanamke huyo alianza kusikia sauti zisizo za kawaida kutoka juu ya ambapo alidhani kuna mnyama ndipo akaamua kuwatuma watoto wake wakubwa kuchunguza na kukutana na mwanaume huyo akiwa amelala juu.

Tracy na mwanaume huyo ambaye jina lake halikuwekwa wazi walikuwa wapenzi miaka 12 iliyopita na waliachana kutokana na mwanaume huyo kuwa na matumizi ya dawa za kulevya kupindukia na wizi ambapo alithubutu kuiba hadi gari la Tracy.

Baada ya matukio ya wizi kuongezeka alikamatwa na kupelekwa gerezani lakini baada ya kutoka alikuwa hana sehemu ya kuishi. Ndipo aliingia kwa siri kwenye nyumba ya Tracy na kujificha kwenye dali.

Hata hivyo baada ya maafisa wa polisi kufika eneo la tukio na kufanya uchunguzi waligundua kuwa mwanaume huyo alitengeneza shimo ili aweze kumchungulia Tracy. Vile vile walikutana na vikombe na machupa yaliyojaa kinyesi pamoja na haja ndogo ikiwa ni ishara kwamba alikuwa anaishi kwa muda mrefu.

Baada ya kugunduliwa, mwanaume huyo alitoroka kabla ya polisi kufika na hakupatikana tena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags