Kim kumrithisha mwanae pete ya almasi

Kim kumrithisha mwanae pete ya almasi

Peter Akaro

Mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian (44) amepanga kumpa mtoto wake wa kwanza, North, 11, pete ya almasi aliyovishwa wakati anachumbiwa na aliyekuwa mume wake, Kanye West (47), ambaye ndoa yao ilidumu kwa miaka sita.

Katika reality show yao, Keeping Up With the Kardashians wiki hii, Kim na dada yake, Khloe Kardashian (40) wanaenda India kwenye harusi na kufichua kuwa kwa bahati mbaya walipoteza almasi moja kwenye mkufu wa Kim alioazima kwa ajili ya shughuli hiyo.

Wakizungumzia tukio hilo katika show hiyo, Kim anaanza kuorodhesha pete zake za zamani alizovishwa wakati akichumbiwa na kusema bado anayo pete ya kwanza alivyovishwa na Kanye West, mshindi wa Grammy mara 24.

Kim ambaye ni mwanzilisha wa chapa ya mavazi ya Skims alisema pete hiyo ipo hadi leo maana hakwenda nayo Paris, Ufaransa mwaka 2016 ambapo alipoteza vito vyake vingi katika tukio la wizi.

"Nakumbuka nilipokuwa na wewe Madison Square Garden, uliniambia nivae pete zote mbili, nilivaa zote na kuzionyesha Instagram. Kanye aliona na kusema, 'usije kuvaa tena pete zako zote mbili kwa wakati mmoja. Je, unataka kuibiwa?," alisema Kim.

Kwa mara ya kwanza Kanye alimvisha Kim pete ya almasi yenye ukubwa wa karati 15 alipokuwa mjamzito wa binti yao wa kwanza, North ambaye sasa ana umri wa miaka 11, na baadaye mwaka 2016 alimpa pete nyingine ya almasi yenye karati 20.

Uhusiano wa Kim na Kanye ulianza Aprili 2012 na kufunga ndoa hapo Mei 2014 huko Florence, Italia, na hadi wanaachana walikuwa wamejaliwa kupata watoto wanne huku wa kwanza North kwa sasa akifanya muziki na filamu.

Kim alisema kwamba walipoenda Paris aliamua kuiacha nyumbani pete hiyo kwa sababu ni ya muhimu kwake na sasa anatarajia kumpa binti yake North ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa watoto maarufu zaidi duniani.

"Na kwa hivyo hii nitaenda kumpa North kwa sababu alikuwepo na mimi wakati nachumbiwa na baada ya kuivishwa aliishika na tukapiga picha pamoja, wakati huo alikuwa na umri wa miezi michache tu," alisema Kim.

Na miezi michache baada ya Kanye kumpa Kim pete nyingine mwaka 2016, mrembo huyo aliibiwa kwa kutumia slaa katika chumba cha hoteli wakati wa Wiki ya Mitindo Paris, kwa ujumla alipoteza vito vyenye thamani ya zaidi ya Dola10 milioni.

Mnamo Aprili 2015 wawili hao walisafiri hadi Yerusalemu ili kubatizwa North katika Kanisa la Mtakatifu James huku Kanye akifichua kuwa awali alifikiria kutoa ujauzito wa North lakini tangu wakati huo amekuwa akipinga vitendo vya utoaji mimba.

Hata hiyo, baada ya miaka sita ya ndoa, Kim aliwasilisha kesi ya talaka hapo Februari 2021, mchakato wa talaka yao ulikamilika rasmi Novemba 2022, na baadaye Kanye alifunga ndoa na Bianca Censori ambaye hapo awali alikuwa mbunifu mkuu wa chapa yake ya mavazi ya Yeezy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags