Mtandao wa kuuza na kusikiliza muziki Spotify imeripotiwa kuwalipa wasanii kiasi cha dola 10 bilioni ikiwa ni zaidi ya Sh 26.5 Trilioni kwa wasanii duniani kote. Huku kiwango hicho kikitajwa kuvunja rekodi.
Malipo hayo ni ya mirabaha ya muziki kwa mwaka 2024 pekee, ambapo kiasi hicho kikiongezwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 10. Kampuni hiyo sasa inakadiriwa kutoa takriban dola bilioni 60 tangu kuanzishwa kwake.
Katika kutoa mirahaba hiyo nao watunzi wa nyimbo na wamiliki wa haki za uchapishaji hawakuachwa nyuma kwani wametengewa kiasi cha dola 4.5 bilioni.
Aidha kwa upande wa msemaji wa Spotify ameweka wazi kuwa mgawanyo wa fedha hizo ni jukumu la lebo za muziki na wachapishaji, hivyo wakishatoa pesa wao hawahusiki kwa lolote.
Kwa upande wa wasanii wa Nigeria wameingiziwa Naira Bilioni 58 ikiwa ni saidi ya Sh 98.5 bilioni, kiasi ambacho ni mara mbili ya mapato ya mwaka 2023 na zaidi ya mara tano ya mapato ya mwaka 2022.
Sehemu kubwa ya mapato hayo imetokana na kupata wasikilizaji wengi wa kimataifa, huku matumizi ya muziki wa Nigeria ndani ya Nchi yakiongezeka kwa 782% katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Leave a Reply