Kauli Ya Basata, Kuhusu Ukimya Tuzo Za Muziki Tanzania 2025

Kauli Ya Basata, Kuhusu Ukimya Tuzo Za Muziki Tanzania 2025

Kati ya maswali yaliyopo kwenye vichwa vya baadhi ya wadau wa muziki nchini ni sintofahamu ya uwepo wa Tuzo za Muziki Tanzania 'TMA' kwa mwaka 2025.

Hii ni baada ya wadau mbalimbali na wapenzi wa burudani ya muziki nchini kuibua hoja kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kuchelewa kutolewa muongozo wa ufanyikaji wa Tuzo za Muziki Tanzania 'TMA' kwa mwaka 2025 ukilinganisha ni miaka mingine hapo nyuma.

Wadau hao wameelekezea wito wao kwa mamlaka husika, ikiwemo Baraza la Sanaa la Taifa 'BASATA' ambao ndio waandaaji na waratibu wakuu wa TMA, kutoa mwongozo kuhusu hatma ya tuzo hizo kwa mwaka 2025.

Utakumbuka, Tuzo za Muziki Tanzania mwaka 2022/2023 zilifanyika mwezi Aprili, na 2024 zilifanyika Septemba. Lakini hadi mwishoni mwa mwezi Julai 2025 hakuna taarifa yoyote kuhusu mchakato wa tuzo hizo, kitu ambacho kinazua mashaka kwa wadau na kudhania huenda zisifanyike kabisa 2025.

Kutokana na hayo Mwananchi imemtafuta Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Kedmon Mapana ambaye amewaomba wadau na wapenzi wa burudani kuwa wavumilivu kwani taarifa za ufanyikaji wa tuzo hizo itatolewa.

"Tutatoa taarifa, kama zisingekuwepo tungekuwa tumeshatoa taarifa kwahiyo wadau na wapenzi wa burudani wawe wavumilivu, hakuna kinachokwamisha," amesema Kedmond Mapana.

Tuzo za muziki Tanzania (TMA) zilianzishwa mwaka 1999 na Baraza la Sanaa la Taifa BASATA ili kutambua vipaji na ubunifu katika kiwanda cha muziki nchini ambapo zilidumu kwa miaka 16, kuanzia 1999 hadi mwaka 2015.

Tuzo hizo hapo awali zilitambulika kama Kilimanjaro Music Awards 'Kili Music Awards' zilirudi tena mwaka 2022 na kutambulika kama Tanzania Music Awards TMA baada ya kutofanyika kwa miaka saba mfululizo tangu mwaka 2015 hadi 2022.

Ukiachilia mbali tuzo hizo kuwa sehemu ya burudani na kutambua vipaji na ubunifu wa kiwanda cha muziki nchini pia zinaonesha namna serikali inavyoshirikiana na kusapoti muziki na vipaji vinavyopatikana nchini, chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags