Vicheko, vilio wasanii walioomba kugombea CCM

Vicheko, vilio wasanii walioomba kugombea CCM

Baadhi ya wasanii nchini waliochukua fomu kugombea majimbo mbalimbali wamewekwa kando na Kamati Kuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku wengine wakichekelea kupenya hatua inayofuata.

Hayo yamesemwa leo Julai 29, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, wakati akitangaza majina ya walioteuliwa na CCM kwenda hatua inayofuata ya kura za maoni za kuwania kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025 mwaka huu.

Kati ya waliopigwa chini ni kaka wa Diamond Platnumz, Rommy Jones 'RJ the DJ' ambaye alichukua fomu katika jimbo la Mbagala, jijini Dar es Salaam, mbali na huyo Abdallah Nzunda 'Mkojani' ambaye alichukua fomu kugombea ubunge jimbo la Temeke naye hajapenya hatua inayofuata.

Mwemba Burton 'Mwijaku' pia hajapenya hatua inayofuata kugombea jimbo la Mvomero Morogoro wengine waliowekwa kando ni waigizaji Stanley Msungu(Kilolo) na Lumole Matovolwa 'Kobisi' (Kibaha Vijijini).
Waliopenya
Baba Levo
Hata hivyo, kati ya waliopenya kwenye chujio hilo ni msanii wa Bongo Fleva Clayton Levocatus 'Baba Levo' ambaye amekuwa miongoni mwa wagombea saba walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini

Babu Tale
Meneja wa nyota wa muziki nchini Diamond Platnumz, Hamisi Shaban Taletale 'Babu Tale'naye ni miongoni mwa wagombea saba walioteuliwa na chama hicho kugombea Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.

Mwana FA

Mwanamuziki na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma 'Mwana FA' amepenya na kuwa miongoni mwa wagombea sita walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kugombea Ubunge Jimbo la Tanga Mheza.

Shilole

Mwanamuziki na mwigizaji Zena Mohamed 'Shilole' na wengine saba walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kugombea Ubunge Viti Maalumu Tabora.

Majina ya wateule hao yametangazwa leo Julai 29,2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags