Fei toto: Hersi akiondoka Yanga narudi kambini hata sasa hivi

Fei toto: Hersi akiondoka Yanga narudi kambini hata sasa hivi

Huku sakata la mchezaji Feisal Salum maarufu kama Fei Toto likiendelea, leo bwana kijana huyo amefunguka mazito baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari na kueleza kuwa.

“Kabla ya mgogoro kuanza, nilikuwa nampigia Ghalib Said Mohamed akawa hapokei simu wala kujibu SMS zangu, baada ya sakata ndipo akanipigia simu sikupokea kwa kuwa niliona ni dharau, mimi masikini sina kitu lakini usinidharau” amesema Feisal

Na kuhusu suala la kurudi katika klabu yake anayoipenda ameeleza kuwa “Sio kwamba namkwepa Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said, nilikutana naye uso kwa uso nikamwambia msimamo wangu, akaniambia nenda CAS"

Anasisitiza "Ikitokea Hersi Said kaondoka Yanga, mimi narudi Yanga hata sasa hivi, sina tatizo na klabu wala mashabiki wa Yanga" amesema Fei Toto


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post