Jol Master: Usioe mwanamke kwa kumuonea huruma

Jol Master: Usioe mwanamke kwa kumuonea huruma

Mchekeshaji na mwigizaji wa filamu nchini, Juma Omary maarufu Jol Master amesema mwanaume hupaswi kuoa kwa mkumbo au kumuonea huruma mwanamke.

Akizungumza na Mwananchi Jol amesema tayari amebahatika kupata mtoto wa kwanza na anaishi na mwanamke, lakini hawajafunga ndoa kwa sababu bado mipango yao haijakaa sawa.

"Sio kila mwenye mtoto ana mke mimi nina mpenzi ambaye tunaishi pamoja. Lakini kwenye suala la ndoa bado tuna mipango yetu kwa hiyo Mungu akisaidia tutafunga ndoa. Ndoa ni kujipanga kiakili kiuchumi na kila kitu, usioe kwa mkumbo au kumuonea huruma mwanamke kwa sababu amekuzalia mimi mwenyewe kuna vitu vyangu vilikuwa kichwani la kwanza ni kupata mtoto," amesema Jol.

Amesema anajisikia vizuri na anajivunia kama kijana kupata mtoto wake wa kwanza wa kiume anayeitwa Genesis.

"Najisikia vizuri sana kwa sababu kupata mtoto ni baraka. Naamini hivyo najivunia siwezi kukataa kama nikiulizwa kama nina mtoto, nasema kabisa tena wa kiume anaitwa Genesis," amesema Jol.

Amesema kama baba alitamani mwanaye aitwe jina la One lakini mama wa mtoto huyo alimwambia wamuite Genesis, jina ambalo linapatikana pia kwenye Biblia.

"Nilikuwa nataka nimuite One kwa maana ya namba moja, nilitaka kumtabiria yeye kuwa namba moja chochote ambacho atakifanya. Lakini mama yake akasema One haijakaa sawa bora tumuite Genesis kwa maana ya mwanzo nikaangalia hata kwenye Biblia jina hilo lipo na halina maana mbaya nikasema poa tumuite," amesema Jol.

Aidha, mchekeshaji huyo ameeleza kuwa anaamini kwenye upendo hata mara baada ya kuondoka ChekaTu na kuanza kujitegemea, kwa kufungua shoo yake ya Zeguy bado anaishi nao kama familia.

"Mimi siamini kwenye ugomvi naamini kwenye upendo. Cheka Tu ni kama nyumbani ulivyotoka nyumbani kwenu kwenda kujitegemea sidhani kama unatoka kwa nia mbaya. Ni kwenda kuanzisha maisha yako, kwa hiyo hata kutoka ChekaTu sijatoka kwa ubaya ndio maana unaona mpaka leo nipo nao kwa sababu ndio kama wazazi wangu" amesema Jol.

Amesema licha ya kupitia magumu baada ya kuanzisha shoo yake ya Zeguy ambayo huusisha zaidi michezo ya jukwaani, bado anaimani watu watamuelewa muda ukifika.

"Chochote kipya lazima kiwe na ugumu. Ni ngumu watu kuelewa kwa mara ya kwanza, kiukweli bado watu hawajaelewa ambacho tunakifanya kwa hiyo ni suala la muda. Muda ukifika itakuwa huwezi kukielezea mara mbili lakini nashukuru kwa mapokezi ya watu mpaka sasa hivi," amesema Jol.ns






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags