Jiongeze: Simba, Yanga kubeba ndoo ya Afrika kabla ya 2030

Jiongeze: Simba, Yanga kubeba ndoo ya Afrika kabla ya 2030

Simba na Yanga zamani waliishia raundi ya kwanza tu. Tena wakipangiwa timu za Waarabu walifungwa kabla ya mechi. Ajabu hivi sasa Waarabu ndo hawataki kukutana na hizi timu za Kariakoo.

 Kwa muda mrefu Simba iliishia robo fainali. Mpaka wakaitwa Mwakarobo na watani zao. Lakini hii leo Simba anapiga fainali. Mwenzake Yanga alifika fainali miaka miwili nyuma. Siyo ishu tena. 

 Kama ilivyo Bongo Movie kubadilika. Pia Simba na Yanga zimebadilika sana. Berkane wanaiogopa Simba. Mamelodi wanaiogopa Yanga. Wydad wananunua mchezaji wa Simba ama Yanga. Yanga inabeba mcheza wa TP Mazembe akiwa na mkataba.

 Ni wazi kwamba Simba na Yanga zimeshavuka daraja la kinyonge. Wako mbali na wala hawana hofu na timu ya Afrika. Waarabu timu za ukanda wa Magharibi na ule wa Kaskazini zinaogopa kukutana na Simba ama Yanga.

 Kabla ya 2030 kuna kombe la Afrika litatua Tanzania. Nani atabeba? Bila shaka ni Simba au Yanga. Hizi timu zimekuwa kubwa sana kwa sasa. Na fainali ya Yanga na MC Alger, Simba na Berkane imeonesha kwamba timu zetu zipo juu na zinaogopwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags