siri ya mafanikio ya Ommy Dimpoz

siri ya mafanikio ya Ommy Dimpoz

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz amesema kuna siri kubwa juu ya maisha yake ambayo watu wengi hawaijui.

Nyota huyo anayetambulishwa na ngoma kadhaa zikiwamo Nai Nai, Baadae, Marry You na nyingine, ameliambia Mwananchi yapo mambo mengi yanaongelewa kuhusu maisha yake. Lakini ukweli sivyo na kwamba sasa ameamua kuanika siri ya mafanikio yake ili wengine wajifunze kupitia kwake.

Dimpoz alisema wapo watu wanaojiuliza kuhusu kuwa kwake maarufu na kudumu katika nafasi hiyo kwa muda mrefu na kwamba siri kubwa ni kujituma na kuwa mvumilivu.

“Yapo mambo mengi, lakini kubwa ni kutokata tamaa. Mimi nikisema ninataka kitu changu, lazima kifanikiwe, huwa sikati tamaa. Kila ninapoanguka huwa ninasimama kisha ninajifuta na kusonga mbele,” amesema Dimpoz na kuongeza;

“Najua nina roho nzuri sana. Sijawahi kuua mtu, sijawahi kudhulumu mtu, nimeshasaidia wengi na wala sijawahi kusema vibaya. Kuanguka ni mambo ya kawaida tu, kwani nami ni binadamu. Jambo jingine ni kwamba kile kidogo ninachopata huwa ninapenda kushea na wengine.”amesema

This story is available exclusively to MWANANCHISCOOP members.
Become a #Scooper and start reading now.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags