Davido atangaza kuacha muziki endapo hatoshinda Grammy 2025

Davido atangaza kuacha muziki endapo hatoshinda Grammy 2025

Staa wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria Davido ameonesha imani yake ya kushinda tuzo ya Grammy usiku wa leo

"Kama sitoshinda Grammy mwaka huu ninafikiria kuacha muziki, nimeweka moyo wangu na roho yangu kwenye kazi, najituma kuliko msanii yeyote ndani ya Africa.

“Daima mimi ndiye huwa mbele naiongoza Afrobeat, naongoza mashambulizi, naitengeneza aina hii ya muziki. Mimi ndiyo jina kubwa kwenye Afrobeat, hilo halina mashaka, lakini kabati langu la tunzo haliakisi machozi, jasho na damu nilivyowekeza.

“Kuchaguliwa kugombea Grammy kwa miaka 2 mfululizo kumenipa furaha, lakini pia hii ni dawa chungu kuimeza. Kama Grammy wangekua kweli wanausawa, ningeshachukua takribani tunzo 20 hadi hivi sasa"amesema Davido

Hata hivyo, Davido ambaye anawania kipengele cha Best African Music Performance ameongeza kuwa mwaka huu anahisi tofauti na Lazima ashinde tuzo yake ya kwanza ya Grammy kwani hakuna kitu kitamzuia.

Sherehe za ugawaji wa tuzo hizo kwa mwaka 2025 zinatarajiwa kufanyika usiku wa leo Februari 2, Los Angeles Crypto Arena.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags