Mwanamuziki kutoka nchini Kenya ambaye alijulikana zaidi kupitia kundi lililovunjika la ‘Sauti Soul’ amefunguka jinsi msanii wa Bongo, Marioo alivyomfundisha mbinu mpya za muziki.
Kupitia kwenye moja ya mahojiano yake aliyoyafanya Bien aliweka wazi kuwa Marioo alimwambia kuwa anajua kuimba lakini atamfundisha namna ya kuwa bora zaidi.
“Marioo aliniambia kuwa naandika nyimbo nzuri, lakini aliniambia kuwa naweza kufanya bora zaidi. Alinifundisha jinsi ya kuandika nyimbo zinazogusa hisia za watu na jinsi ya kuwasilisha ujumbe wangu kwa ufanisi zaidi,” alisema Bien
Mbali na hilo Bien alimshukuru Marioo kupitia ushirikiano wao wa ngoma ya ‘Nairobi’ akidai kuwa ushirikiano huo umembadilishia maisha yake huku akimtaja Darasa na Marioo kuwa wasanii anaowakubali zaidi.
Nairobi kutoka kwa Marioo na Bien umekuwa wimbo ambao umewavutia wengi ukitoka kwenye album ya Bad iitwayo ‘The God Son’ ambapo wimbo huo mpaka kufikia sasa umeshatazwamwa na zaidi ya watu milioni 5.
Leave a Reply