Leo Februari 2, 2025 zinatarajiwa kugawiwa tuzo za Grammy ambazo zitakuwa za 67 kufanyika tangu kuanzishwa kwake Mei 4, 1959.
1. Tuzo za Grammy ambazo zinaangazia wasanii waliofanya vizuri mwaka 2024 zina jumla ya vipengele 94 ikiwa ni tuzo zenye vipengele vingi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mara ya mwisho tuzo hizo kuwa na vipengele vingi ni 2010 ambapo zilikuwa na jumla ya vipengele 109.
2. Beyonce akiwa anashikilia rekodi ya msanii anayeongoza kuwania tuzo hizo kwa mara 99 pia ndiyo msanii anayeshikilia rekodi ya msanii aliyechukua tuzo hizo mara nyingi zaidi akibeba mara 32 ndani ya miaka tofauti tofauti.
Anafuatiwa na Quincy Jones (28), Jay Z & Kanye West (24), Kendrick Lamar (17), Eminem (15), Andre 3000 (9), Dr. Dre (7), kundi la Outkast (6), Drake (5), na Lil Wayne (5).
Licha ya Beyonce kutoa albamu nyingi zilizofanya vizuri duniani, hajawahi kushinda kipengele cha albumu bora ya mwaka.
Ikumbukwe ametoa nane za studio, albamu tano za moja kwa moja LIVE Album, albamu tatu za mkusanyiko, EP tano, albamu moja ya sauti na albamu mbili za karaoke.
Ameuza zaidi ya rekodi milioni 200 duniani kote, na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wa muziki wanaouza zaidi wakati wote.
Wakati wa sherehe za Grammy 2024, Jay-Z ambaye ni mume wake alihutubia akiwaambia watazamaji. "Sitaki kumwaibisha binti huyu, lakini ana Grammys nyingi kuliko kila mtu na hajawahi kushinda albamu bora ya mwaka”.
Marehemu Quincy Jones ambaye alikuwa mtayarishaji nguli wa muziki duniani akifanya kazi kwa ukaribu na Michael Jackson, hajawahi kuimba lakini anamiliki tuzo nyingi za Grammy akishinda mara 28.
Wakati Beyonce akiwa ndiye kinara kwa wasanii wenye tuzo nyingi za Grammy duniani akiwa ameshinda mara 32, kuna huyu mtayarishaji nguli wa muziki duniani Quincy Jones ambaye ana tuzo 28 za Grammy huku akiwa amechaguliwa kuwania mara 80.
4. Ngoma ya Not Like Us ya kwake Kendrick Lamar inawania vipengele vitano kwenye tuzo za Grammy 2024, teuzi hizo ni pamoja na Rekodi bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka, wimbo Bora wa kutumbuiza wa Rap, Wimbo Bora wa Rap, Video Bora ya Muziki.
Lamar ameimarisha hadhi yake kama nyota wa kimataifa ambapo katika kipindi chote cha kazi yake amepokea uteuzi wa GRAMMY mara 57, akishinda 17, na kumfanya kuwa mmoja wa rappers waliobeba zaidi zaidi tuzo hizo katika historia ya GRAMMY.
5. Wasanii kutokea Afrika waliofanikiwa kupenya kwenye teuzi za Tuzo hizo ni pamoja na Rema akiwania Best Global album 'Heis', Burna Boy akiwania Best African Music Perfomance kupitia wimbo wa Higher, Yemi Alade akiwania Best African Music Perfomance kupitia wimbo 'Tomorrow' .
Asake akiwania Best African Music Perfomance kupitia wimbo MMS, Wizkid akiwania Best African Music Perfomance kupitia wimbo MMS, Tems akiwania Best African Music Perfomance kupitia wimbo Love Me JeJe na Best global album kupitia album ya 'Born In The Wild' , Davido na Lojay.
6.Will Smith atashiriki Tuzo za Grammy ikiwa ni tuzo kubwa ya kwanza baada ya kupigwa marufuku ya kutoshiriki tamasha lolote kwa miaka 10 baada ya kumpiga Kofi mcheshi Chris Rock wakati wa ugawaji wa Tuzo za 94 za Oscar Mnamo Machi 27, 2022.
Kofi hilo lilitokana na utani ambao Rock aliufanya kuhusu aliyekuwa mke wa Smith, Jada Pinkett Smith. .
Imethibitishwa kuwa, Smith atapanda jukwaani kwenye Ukumbi wa Crypto.com huko Los Angeles zinapofanyika Tuzo za 67 za Grammy leo Februari 2, 2025.
Smith ni mmoja wa watu maarufu walioteuliwa kuwasilisha kwenye hafla hiyo ya kila mwaka iliyojaa nyota, huku Taylor Swift na Queen Latifah wakiwa miongoni mwa majina yatakayotambulisha tuzo usiku wa leo.
Leave a Reply