Msanii wa Bongofleva Harmonize ametangaza kuachia wimbo Ijumaa hii ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kuwaimbia wapenzi wa zamani.
Katika wimbo huo amesema anaomba mashabiki zake wasiwajumuishe Ma Ex aliyowahi kutoka nao akiwemo Kajala, Poshy Queen na wengineo kwani wimbo huo sio kwa ajili yake tu bali kwa ma ex wote duniani.
"Haihusiana na ex wangu yeyote ninaheshima kubwa sana kwao wote, kama nikimuhitaji Ex wangu yeyote haitokuwa kazi ngumu kama mnavyodhani !! ila ndiyo siwezi upendo wangu unapitiliza nakuwa kama kaka mkubwa kwenye familia.
“So hata ikitokea tumeshindwa heshima na adabu yangu kwenye familia inabaki palepale so ex hata akaninunia tunakutana kwenye vikao vya familia hili goma ni kwa niaba ya ex wetu wote duniani nisingependa kuona mnawataja wakwangu tu kisa nimeimba" ameandika Harmonize.
Hata hivyo, Harmonize aliongezea kuwa hana shida na alieyekuwa mpenzi wake Kajala .
"Kimsingi hajanikosea chochote na hamnaga hasira za miaka mitatu utakuwa uchawi huo. Tulitupiana maneno kadhaa kama ilivyo kawaida yangu mimi nakuwaga mtoto mkubwa kwenye familia nilimfuata mama Kajala nikamuomba msamaha kwa kilichotokea akaniambia usijali mwanangu akanipikia ugali nikala nikalala na usingizi jioni tukapiga stori mbili tatu na mzee Masanja so we Good sitaki kusikia hii mada tena" ameandika Harmonize.
Leave a Reply