Anjella amefunguka sababu ya ukimya wake

Anjella amefunguka sababu ya ukimya wake

Kumekuwa na minong’ono mingi kuhusiana na mwanamuziki wa bongo fleva Anjella kuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa nyimbo, mwanadada huyo ameeleza sababu ya ukumya wake bila kutoa nyimbo na kueleza kuwa alikuwa anajitibia tatizo lake la mguu kwa muda wote huo kwani mguu wake ulikuwa tayari umeanza kuonesha dalili zisizo nzuri.

 “Nilikuwa nahangaika na matibabu ya mguu kwasababu ulikuwa tayari umeanza kuwasha na kutoa malengelenge, ikanibidi niwahi Hospitali ili usiniletee matatizo mengine” alisema Anjella.

Pia msanii huyo ambaye kwa sasa anajisimamia yeye mwenyewe kama msanii wa kujitegemea ameachia wimbo wake mpya hii leo “Blessing” ambao unaelezea hustle zake za maisha ya muziki pamoja na sababu za kutemwa Konde Gang.

Aidha kwenye moja ya mashairi yake amesema muziki kwake ulikuwa ni ndoto na hakuitimiza kwa kulala, kipindi anajitafuta akajiunga na lebo ya Konde Gang ilimradi awe imara.

Maisha ya gwaride yalipoanza hapo ndipo alinyoosha mikono juu na kushindwa kuendelea na lebo hiyo kutokana na matatizo ya mguu na ndio sababu ya kuachwa na kunyamazishwa mdomo.

Kiuhalisia Angella halaumu alikopita kwani amesema njia hiyo haikuwa mbaya na atakuwa ana kufuru endapo atasema haikumfisha popote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags