Anjella aeleza magumu yaliomkuta baada ya kuondoka Konde Gang

Anjella aeleza magumu yaliomkuta baada ya kuondoka Konde Gang

Mwanadada ambae anatamba kupitia nyimbo yake ya Blessing, Anjella amefunguka mazito ambayo yalimpata baada ya kuondoka katika Lebo ya msanii mkubwa Tanzania, Harmonize ya Konde Gang.

Anjella ameyaeleza hayo kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari nchini na kueleza mambo yote ambayo amekumbana nayo mfano kuzimia baada ya kuvunjiwa mkataba.

“Baada ya kutoka Konde Gang kiukweli sikuwa na muelekeo nilikata tamaa na kupoteza tumaini, ashukuriwe Mungu wakati ambao nawaza itakuwaje nikamkubuka mtu mmoja anaitwa Zungu yeye ndio alinipa Moyo na kuniambia sipo sawa na akanitafutia Mwanasaikolojia nikaambiwa nisiende Studio mpaka nitakapo kaa sawa” aliendelea kwa kusema

“Na wakati ule kwenye mitandao kulikuwa na mambo mengi ilikuwa nikiona ninavyosemwa nilikuwa nazimia kila muda mpaka akanipokonya simu ili nisione yanayoendelea mitandaoni, Baada ya kukaa sawa akanikutanisha na Kontawa ndio tukaandika wimbo” amesema Anjella

Sababu kuu ambayo ilimfanya mwanadada huyo sababu kubwa iliyofanya Lebo hiyo kuvunja mkataba nae ilikuwa ni kuchelewesha kuwasilisha kazi (Album) na kipindi hicho alikuwa anaumwa hivyo alishindwa kufanya hivyo.

Mbali na hayo amefunguka kuwa Kipato kikubwa alichowahi kupokea kutokana na kazi zake ni Sh.Milioni 4 ambazo zililimbikizwa kwa muda wa miezi 3 au 4 ndio akapata kiasi hicho. Huku akiweka wazi kuwa mkataba wake alikuwa anapokea asilimia 40 kwa kila kazi aliokuwa anafanya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags