Zuchu na Diamond penzi shatashata

Zuchu na Diamond penzi shatashata

Nyieeee unaambiwa usinene ukamara bwana, kumbuka kuweka akiba ya maneno, pia usiseme sana bwana, mambo yameanza kutaradadi kupitia mitandao ya kijamii bwana ambapo kumesambaa baadhi picha zikiwaonesha mastaa wawili pamoja.

Aloooh, akiwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, msanii Zuchu bado salamu za kumtakia kheri zinaendelea bwana, huu hapa ujumbe kutoka kwa boss wake Diamond platnumz katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.

Boss kama boss aliandika waraka takatifu kupitia ukurasa wake wa Instagram na mambo yalikuwa hivi;

''This week we commemorate and celebrate the reborn of the gifted, creative, loving, talented, and humble girl that Tanzania has been blessed with  @officialzuchu ...Thank you for continue making Wasafi, Swahilis, Women and the whole African continent proud...ni faraja kuona ulipoanzia hadi sasa kufikia kuwa miongoni wa Icons kwenye Bara la Africa.. Siku zote kumbuka, kila kazi ina mitihani na changamoto zake....jitahidi kuipokea kila inapokuja na kutafta njia sahihi ya kuishinda, maana tafsiri sahihi ya mtihani ni Kupanda daraja baada ya kufauru...Mwenyez Mungu akupe baraka na akulinde katika Maisha na safari yako hii ya kuchangia kuonesha Dunia kua WaAfrica tumebarikiwa kipaji kias gani… Remember Lion Loves you always ๐ŸŒนโค๏ธ๐ŸŽ‚๐Ÿพ'' 

Maneno hayo yaliambatana na slides ya picha na video mbalimbali za Zuchu akiwa pamoja na Diamond wakiweza wazi mahaba mazito walikuwa nayo. Hizi picha na video nizo hasa zilizozua gumzo kubwa na kuvunja ukimya juu ya uhusiano wao ambapo mashabiki wengi walicomment kwa kukubali kuwa wamepigia mstari tetesi ya kuwa wawili hao ni wapenzi.

Ebwana eeeh!!! Unaweza dondosha comment yako hapo chini mdau kuhusu jambo hili wewe unalionaje?.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post