Zuchu aongoza kusikilizwa Spotify 2024, upande wa wanawake

Zuchu aongoza kusikilizwa Spotify 2024, upande wa wanawake

Mwanamuziki anayetamba na wimbo wa ‘Wale Wale’ aliyomshirikisha Diamond, Zuchu ametajwa kuongozwa kusikilizwa katika mtandao wa Spotify kwa upande wa wanawake.

Zuchu ametajwa kuwa kinara kwa wasanii wa kike kutokana na kuendelea kutia alama katika muziki wa Bongo Fleva huku wasanii wengine wanaosikilizwa zaidi ni pamoja na Nandy na Phina.

Tangu kutambulishwa kwake katika lebo wa WCB mwaka 2021 Zuchu amekuwa akiachia ngoma ambazo zinapenya zaidi ndani na nje ya nchi ikiwemo Sukari, Siji, Antena, Zawadi, Napambana na nyinginezo.

Mbali na kutajwa kuwa msanii anayesikilizwa zaidi lakini pia nyimbo zake mbili zimeripotiwa kusikilizwa zaidi ikiwemo Siji aliyomshirikisha Toss na Zawadi aliyomshirikisha Dadiposlim.

Aidha kwa upande wa wasanii wakiume wanaoongiza kusikilizwa ndani ya Tanzania namba moja imeshikiliwa na Chris Brown wa pili akiwa Marioo na watatu Diamond.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags