Mazoezi ni moja kati ya vitu muhimu vya kufanya kwa mwanadumu kwani tunaelezwa leo licha ya faida hiyo lanipi pia udsaisia kuongeza nguvu za kiumme.
Mratibu wa Lishe Manispaa ya Temeke Dk. Charles Malale akizungmza na Mwananchi Scoop amefunguka mambo mbalimbali hasa kuhusiana na maoezi ambayo mtu anaweza kuyafanya ili kuongeza nguvu za kiume.
Dk. Malale alisema moja ya mazoezi hayo ni kutembea kwa miguu
Alisema kutembea ni moja ya zoezi zuri kabisa ambalo mtu anaweza kulifanya na linaweza kufanywa mahali popote, wakati wowote na haligharimu chochote.
“Sehemu nzuri za kutembea ni nje au uwanjani au karibu na msitu ambako unaweza kupata hewa safi ya asili ya kutosha. Unaweza kufanya ndiyo zoezi lako la kwanza asubuhi au jioni vilevile mchana wakati wa jua kali ni muda mzuri kufanya zoezi hili au wakati mwingine wowote utakapojisikia kufanya basi fanya kuliko kuleta visingizio,” alisema.
Aidha alisema kama unahitaji kupunguza uzito basi amewashauri kutembea mwendokasi kidogo dakika 60 bila kusimama mara moja mpaka mbili kila siku.
“Huhitaji kusema nitoke hapa mpaka pale, unahitaji uwe na saa mkononi kukuonyesha kwamba kweli dakika 60 zimeisha ukitembea pasipo kusimama,” alisema
Alisema kama afya ya mtu siyo nzuri anaweza kuanza hata na dakika 15 siku ya kwanza huku akiongeza dakika 5 zaidi kila siku mpaka utakapozoea kwenda dakika 60 pasipo kusimama basi uendelee hivyo kila siku.
“Hivyo kama utatembea lisaa limoja asubuhi na lisa linguine jioni ina maana mwili wako utabaki unachoma mafuta kwa masaa yote 24 katika siku! Na matokeo yake ni kuwa hatutasikia tatizo la kitambi au unene kupita kwako tena.
“Ukiacha kuchoma mafuta zoezi hili pia linaongeza msukumo wa damu kwenda mishipa karibu yote katika mwili wako na hivyo moja kwa moja kuhusika na kukuongezea nguvu za kiume na kukuwezesha kuhimili tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi,” alisema
Kuchuchumaa na Kusimama
Alisema kuchuchumaa na kusimama ni zoezi gumu kulifanya lakini mtu akilizoea na kulifanya mara kwa mara basi hatachelewa kuona faida zake.
“Hili ni zoezi linalotengeneza na kuimarisha misuli katika eneo lako lote la chini ya mwili kuanzia misuli ya tumbo (sixpacks), mgongoni mpaka misuli ya kwenye visigino miguuni.
“Ukizoea kufanya zoezi hili sahau kusumbuliwa na kitambi na unaweza kutengeneza misuli ya tumboni maarufu kama ‘sixpack’ kirahisi zaidi. Zoezi hili pia husadia kuchoma mafuta mwilini ingawa siyo sana kama vile kukimbia au kutembea mwendokasi lisaa lizima,” alisema.
Alisema anachotakiwa kufanya mtu ni kuchuchumaa na kusimama mara 15 au mpaka 25 huku akipumzika sekunde 30 au dakika 1 kisha anaendelea tena kwa mizunguko mitano.
“Kama ni ngumu sana wakati unaanza unaweza kuanza na kuchuchumaa na kusimama mara 5 au 7 kisha pumzika huku ukiendelea kuongeza idadi hivyo hivyo kidogo kidogo mpaka utakapozoea kwenda mara 25 bila kupumzika.
“Unaweza kufanya zoezi hili mahali popote iwe ni chumbani, jikoni, ofisini na mahali pengine popote. Unaweza kufanya mara 3 au 2 kwa siku. Ukiona unapungua zaidi uzito punguza mpaka mara 1 tu kwa sik,” alisema
Alisema zoezi hilo linaongeza msukumo wa damu katika sehemu zote za mwili na wakati wote huku faida nzuri zaidi ya zoezi kuliko mengine yote ni kuwa inaifanya damu iliyokuwa imeenda miguuni kurudi tena juu katika moyo na mwili kwa ujumla jambo ambalo ni mhimu katika kusafisha damu na itembee kwa uhuru wote kila sehemu.
Dk. Malale alisema kwa mtu anayefanya kazi za ofisini na anakuwa amekaa kwenye kiti masaa mengi basi ajuwe damu yake inajilundika miguuni na haipati nafasi ya kurudi juu isafishike na kuongeza mzunguko.
“Matokeo yake utaanza kuona miguu au nyayo zako zinaanza kuwaka moto au miguu inavimba au miguu tu inauma kutokana na hiyo damu ambayo imejilundika na kutengeneza taka za asidi ambazo mwisho wake kabisa hutokea kuwa kansa,” alisema na kuongeza
“Zoezi hili hujulikana pia kama ‘squatting’ kwa Kiingereza siyo tu linaongeza msukumo wa damu mwilini lakini pia linaongeza na kuweka sawa homoni mhimu sana ya kiume ijulikanayo kama ‘testosterone’ na matokeo yake utaongezeka nguvu zako za kiume kwa haraka zaidi ndani ya siku kadhaa tu na utajisikia raha sana unapofika kileleni tofauti na siku zingine kama utaanza kufanya zoezi hili,” alisema
Alisema nguvu za kiume zinatengenenezwa kwenye magoti na kwenye enka karibu na visigino chini.
“Hivyo zoezi lolote litakalozifanya sehemu hizi mbili zishughulishwe lazima moja kwa moja litapelekea kuongezeka kwa nguvu za kiume. Kuthibitisha hili mwanagalie magotini mtu aliyezoea kupiga punyeto utaona waziwazi eneo hilo linang’aa na ni dhaifu kwa macho tu!,”
Kufanya mazoezi ya viungo
Alisema kama mwanaume anahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, anahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.
Aidha alisema kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’.
Anaongeza kusema vitu vingine vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni pamoja na magonjwa kama vile ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la juu la damu.
Wengine wenye hatari ya kupatwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ni pamoja na wanaume wenye shinikizo la juu la damu, wenye matatizo ya tezi, waliowahi kufanya upasuaji katika viungo vya uzazi.
Leave a Reply