Wema Sepetu: Najali furaha yangu

Wema Sepetu: Najali furaha yangu

Mambo mengi  muda ni mchache, yaani ukisinzia kidogo tu unapitwa aisee! Wakati wasanii wengine wakidai talaka huku wengine wanazama kwenye dimbwi la malavidavi na baadhi wanaoa na kuolewa.

Ebwana mtandaoni sio pouwa comment zimekuwa nyingi na kila mtu anazungumza lake baada ya video ya Tanzanian sweetheart Wema Sepetu kwenye malavidavi na mpenzi wake Whozu kwenye usiku wa kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.

Basi bhana walimwengu hawakosi la kusema na wakaliwa jambo likiwa bado la moto na mjadala mkubwa unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na penzi hilo jipya la wawili hao, basi bila kuchelewa madam Wema akajibu mashambulizi kwa wanaomsema kuhusu penzi lake na msanii Whozu na kusema Kwasasa  anachojali ni furaha yake kwani ameishi maisha yakutokuwa na furaha kwa muda mrefu na amekuwa na furaha sana toka akutane na mpenzi wake, pia hatojali maneno ya watu kuhusu mahusiano yake.

Mmmmmh! Hatari mambo ya malavidavi waswahili wanasema hayanaga mshauri, dondosha comment yako hapo chini je ni sahihi kusikiliza maneno ya watu ukiwa kwenye mahusiano?

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags