Waziri apigwa risasi na mlinzi wake.

Waziri apigwa risasi na mlinzi wake.

Waziri wa kazi, Ajira na uhusiano wa viwanda Nchini Uganda, Charles Okello Engola ameuawa asubuhi hii kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake.

Spika wa Bunge nchini humo Anitha Among amethibitisha kifo hicho bungeni leo amesema. "Asubuhi hii nimepokea taarifa za huzuni kuwa Mh. Engola amepigwa risasi na mlinzi wake ambaye pia amejipiga risasi,  hatuwezi kubadili chochote ni mpango wa Mungu," Among amesema.

Tukio hilo limetokea asubuhi hii ambapo imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwenda kazini ambapo ghafla mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia Mtaani.

Majirani wamesema mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi na Waziri huyo.

Sambamba na hayo inaripotiwa kuwa mlinzi huyo baadaye aliingia saluni moja iliyopo jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags