Wasanii waliobamba kwenye harusi ya Wolper

Wasanii waliobamba kwenye harusi ya Wolper

Its Friday watu wangu wa nguvu, basi bwana weee, wiki hii kwenye fashion mambo ni moto, mambo ni firee watoto wa mjini wanasema hivyo.

Yap ndani ya kipengele cha Fashion wiki hii tutaangazia mastaa waliodamshi kwenye halfa ya harusi ya muigizaji Jacqueline Wolper.

Kama unafahamu hii wiki imeanza na mambo kadha wa kadha hususani harusi ya muigizaji maarufu hapa nchini Wolper aliyefunga na mwanamitindo anayefahamika kama Rich mitindo.

Ebwana kama hukubahatika kushuhudia tukio hilo kupitia mitandao ya kijamii basi acha nikupe update ya yale yaliyojiri kwenye hafla hiyo.

Mwigizaji Wolper, sasa rasmi anatambulika kama Mrs. Richard Samweli Bruno na hii ni baada ya kufunga ndoa na Mwanamitindo Richard Bruno.

Ikumbukwe kuwa mwigizaji Jacqueline Massawe “Wolper” na Mumewe Rich Mitindo wamefunga ndoa yao tarehe 20 November katika Kanisa la St. Peter’s Dar es Salaam.

Baada ya kufunga ndoa hiyo ambayo kwenye sherehe za kuwapongeza wawili hao zilizohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa bongo movie, bongo fleva, bila kusahau watu mbalimbali.

Aloooh ngoja nikuambie sasa baadhi ya  mastaa ambao waliweza kujitokeza kwenye hafla hiyo akiwemo mrembo Wema Sepetu, Irene Uwoya, Hamisa Mobetto, Nandy bila kumsahau mumewe Billnass, Petitman Wakuache, Zamaradi Mketema na wengine wengi.
 

Ukiachana na waliohudhuria, kwenye kipengele cha fashion leo tutaangazia wasanii waliolipuka au kubamba ama unaweza kusema waliodamshi kwenye hafla hiyo.

Mwanachi Scoop magazine imeshare baadhi ya picha za mastaa hao kisha na wewe utatafakari kwa upande wako na bila shaka utakua unaendelea kupata elimu juu ya mavazi ya ukumbini bwana.

Yes, Ijumaa ni siku ya kujiburudisha na kupumzika basi kwenye fashion nakuachia uweze kutazama mavazi ya ukumbini bwana kuwa makini usije kuabika kwenye kumbi za watu.

Alooooooooh kila la kheri mtu wangu, Enjoy kipengele chetu pendwa kabisaa cha fashion bila kusahau urembo, bye bye!!!!.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags