Wasanii wa bongo kwenye tuzo za The Headies

Wasanii wa bongo kwenye tuzo za The Headies

Oyaaaa! wanangu vipi kweli hii julai ni yetu au tunyamaze tu kwanza, basi bwana ukiaachana na kuipania number one trending kuna hii kubwa kuliko ni kuhusian na waandaji wa Tuzo za The Headies kutoka nchini Nigeria wameweka wazi majina ya wanaowania Tuzo hizo kwa mwaka 2023, huku wasanii watatu pekee kutoka nchini Tanzania ndio wamepata nafasi ya kutajwa mwaka huu.


Wasanii hao wakiwa ni Zuchu kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka Afrika Mashariki ambapo anawania na aliyekuwa msanii mwenza katika lebo ya WCB Rayvanny , Eddy Kenzo, Hewan Gebreworld pamoja na boss wake Diamond Platnumz.

Simba pia ametajwa kwenye kipengele cha African Artiste of The Year akichuana na The African Giant Burna Boy, Marwa Loud, Rema na Black Sherrif. Huku Rapper na Mfanyabiashara Love maarufu Diddy atatunukiwa Tuzo ya Heshima.

Wasanii wengine ambao wamebahatika kuingia katika tuzo hizo ni The late Costa Titch, Davido, Drake, Future, Ed Sheeran, Selena Gomez, Asake ambaye ametokea mara nane katika Tuzo hizo na wengine wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags