Wanasoka wanaomiliki ndege binafsi zenye thamani zaidi

Wanasoka wanaomiliki ndege binafsi zenye thamani zaidi

Baadhi ya watu maarufu duniani wamekuwa wakitamani na wengine kuwekeza kwenye umiliki wa ndege binafsi, wapo baadhi ya wanamuziki ambao tayari wanamikili vyombo hivyo vya usafiri lakini kwa wanasoka nao wanaonekana kuwa na mapenzi makubwa kwa ndege binafsi.

kati ya wanasoka maarufu duniani wanaomiliki ndege binafsi za thamani ni Cristiano Ronaldo mchezaji wa klabu ya Al Nassr ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi naye anamiliki ndege ya Gulfstream G650, yenye thamani ya takribani dola milioni 73 ambazo ni zaidi ya tsh 183.6 bilioni



Mchezaji wa Inter Miami Lionel Messi, naye anamiliki GV ya Gulfstream, ambayo aliinunua kwa zaidi ya dola milioni 48, ambazo ni zaidi ya tsh 120.7 bilioni, ndege hiyo ina viti 16 ambavyo vinauwezo wa kubadilika na kuwa vitanda nane.



Zlatan Ibrahimović ambaye ni mchezaji wa zamani wa Sweden aliyecheza kama mshambuliaji yeye anamiliki ndege aina ya Sesna Citation Longitude yenye thamani ya $26,000,000 mbayo ni zaidi ya tsh 65.3 bilioni


Aidha Paul Pogba mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anachezea klabu ya Serie A Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, ambaye kwa sasa amesimamishwa kuingia mchezoni, yeye anamiliki ndege binafsi ya Gulf Stream G 280 ambayo ina thamani ya $ 21,000,000 ambayo ni zaidi ya tsh 52.8 bilioni




Pia David Beckham mchezaji wa zamani wa kulipwa wa Uingereza, ambaye ni rais wa sasa na mmiliki mwenza wa Inter Miami na wa Salford City yeye pia anamiliki ndege binafsi aina ya Bombardier challenger 350 yenye thamani ya $21,000,000 ambazo ni zaidi ya tsh 52.8 bilioni






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags