Idara ya Usalama ya kitaifa nchini Urusi, FSB imesema imewaweka kizuizini raia watano wa Urusi, watatu wa Ukraine na mmoja wa Armenia kwa kuhusika na mlipuko ulioharibu daraja linaloiunganisha na Rasi ya Crimea Jumamosi iliyopita.
FSB imesema mlipuko huo ulipangwa na idara ya ujasusi ya jeshi la Ukraine pamoja na mkurugenzi wake Kyrylo Budanov na kifaa kilichotumika kulipulia kilitoka Ukraine hadi Urusi kupitia Bulgaria, Georgia na Armenia.
Aidha FSB iliyochukua mikoba ya lililokuwa shirika la ujasusi la enzi ya Kisovieti, KGB, pia imesema kwamba ilizuia mashambulizi ya Ukraine katika miji ya Moscow na Bryansk.
Hadi sasa Ukraine haijakiri rasmi kuhusika na shambulizi hilo, ingawa baadhi ya maafisa wa Ukraine walionekana kufurahia mlipuko huo.
Leave a Reply