Wajue baadhi ya mastaa waliobeba mimba mwaka huu

Wajue baadhi ya mastaa waliobeba mimba mwaka huu

Hahahahah! Make hapa kwanza ncheke, maana mwaka huu nchini kwetu tumeongezeka ghafla au ndo baridi limezidi, hahaha watoto wa mjini wanakamsemo kao bwana, ‘wakati wengine wakiwaza kulima mashamba, wengine wanalimana miili’ oooohooo jokes bwana watu wangu wa nguvu.

Week hii kwenye burudani bwana kama kawaida yetu tunakusogezea vile vitu moyo unapenda. Sasa leo tumekuja na wale mastaa ambao mwaka huu bwana wamebarikiwa kushika mimba, vijana wa mjini wanaita vibendi, naona waigizaji kama walipania sana maana sio pouwa yaani kama wametuamulia hivi.

Alooooh! Sasa hapa tunaanza na yule mwanadada mkongwe kabisa katika tasnia ya bongo movie na mwanamitindo mashuhuri Jacqueline Wolper au Mama P ambae alipata bahati ya kupata mtoto wake wa pili aliejifungua miezi kadhaa iliopita. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, muigizaji huyo aliposti picha ya mtoto wake wa kike kwa mara ya kwanza na kuandika kuwa,

“Malikia wa baba yake na mama yake katoka kanisani katika siku yake ya 40, kiss you queen.”

Eeeebwanaaweee! Wambea kama wambea tulijua kufungwa midomo maana maneno yalikuwa mengi kuhusiana na wawili hawa kutokufika mbali lakini Mungu kawaangaza mchana kweupee!

Uwiiiiii! Ukiachana mke ya mwanamitindo maarufu bwana, kuna huyu binti wa kichaga alituficha sana lakini waswahili tuna kamsemo ketu bwana kuwa ‘pembe la ng’ombe halijifichi’ na kweli bwana siku ya siku akaona ya nini wacha niliachie.

Ni msanii wa bongo fleva na muigizaji pia Faustine Mfinanga maarufu kama Nandy nae ni moja ya masuper star ambao kwa mwaka huu wamebahatika kupata ujauzito na week kadhaa zilizo pita alitambulisha rasmi jinsia ya mwanae licha ya kusema kuwa hata weka wazi jinsia ya mwanae wala jina lakini kauli hiyo ilibadilika baada ya kujifungua kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka kwa kuandika kuwa

“Kwanza kabisa namshukuru Mungu wangu kwa ukuu wake hakika amezaliwa binti wa kichaga, nakupenda sana umenionesha umuhimu na ugumu wa kukamilisha kuitwa mama na kumalizia kwa kuandika asante mume wangu kwa zawadi hii, nashukuru kwa kunipa best friend.” ameandika mwanadada Nandy.

Alooooh! Tunaendelea kulisakata gurudumu bwana, tunakusogezea mwanadada mwenye kitimtim chake mjini, Gladness Kifaluka maarufu kama Pili kitimtim. Basi bwana niwaibie siri inasemekana yeye ni shoga mkubwa wa mke wa Nenga na wamepata mimba siku moja na besti yake huyo.

Pili Kitimtim inavyosemekana bwana nae amejifungua lakini hajaweka wazi jinsia wala picha ya mtoto wake lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram aliposti video kipindi cha ujauzito wake na kuandika kuwa

 “Msichoke najikumbushia enzi zangu, yaani nikikumbuka hichi kipindi jamani natetemeka,” ameandika Pili nyie nyie hii ina maanisha kama mzigo umeshashuka tusubiri tu jina na picha la mtoto wake.

Hatujamalizaaa hatujamalizaa! Yaani kuwaletea habari nzuri kama hizi siwezi acha labda mniue, basi bwana tunaendelea na mwanadada ambae anatingisha sana katika tamthilia ya Jua Kali. Zaiylissa au watu wanamfahamu kwa jina Naira Juakali, nae bwana alibahatika kupata ujauzito na kufanikiwa kujifungua mtoto wa kike lakini mtoto alipoteza kwa bahati mbaya.

Naira kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka wazi kuhusiana na kifo cha binti yake na yale yote aliyokumbana nayo wakati wa ujauzito wake, kuhusiana na mwanaume aliempa ujauzito kumfanyia mambo yakikatili jambo ambalo lilizua taharuki katika mitandao ya kijamii.

Tuseme tu innallilllah wainnallillah rajiun, allah atamjaalia mtoto mwingine huenda huyu hakuwa rizki yake.

Sasa leo naona tutamatishe na huyu binti ambae kipaji chake cha kuigiza alianza kitambo sana yaani naweza kusema ni mdogo kiumri lakini ni mkongwe katika tasnia ya uigizaji Warda maarufu kama Tahiya wa kombolela, alifanya maajabu sana katika tamthilia hiyo.

Licha ya kuwa na ujauzito lakini alicheza uhusika wake kama ilivyo mtaka bila kuchoka, binti huyo bwana alifanikiwa kupata ujauzito na kujifungua mtoto wa kike ambae alipa jina la “Aygul.”

Ooohoooo! Naona kwa leo tuishie hapo watu wangu wa nguvu hata kesho nayo ni siku, usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa mastori kemkem kama haya mwanangu sana. Kama kauli mbiu yetu inavyosema hatunaga mbambamba, yaani tunakupa vile vitu vya motrooo.

Usikose kufuatilia magazine ya next week maana ntakusogezea unyama wa makala moja matata sana ya burudani. Embu dondosha komenti yako hapo chini ni star gani ambae tumemsahau katika listi hii.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post