Wachezaji 10 bora wa soka wanaofuatiliwa zaidi duniani

Wachezaji 10 bora wa soka wanaofuatiliwa zaidi duniani

Oooooooooh! Another furahi day wanangu sana, kama kawaida yetu katika segment yetu ya burudani hatujawahi kufeli. Sasa leo tunakusogeza hadi nje ya Tanzania kushuhudia wale wachezaji bora 10 ambao hukubalika, kutazamwa na kupendwa na watu wa kila rika. Yaani hapa  nazungumzia wale wajuu kabisa ukiachana na  Mayele, Chama, Bocco na Feitoto.

Kama mnavyojua soka la mpira wa miguu ndilo lenye wafuasi wengi duniani kuliko mchezo wowote, hapo awali kabla ya kuja wachezaji wengine kulikuwa na maswali mengi kwa mashabiki ulimwenguni kuwafananisha magwiji hawa wawili Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. 

Hapa tunaenda kutathmini wachezaji 10 bora wa kandanda ambao kila mmoja wao anaweza kuzingatiwa kama mwanasoka bora zaidi ulimwenguni kwasababu kila mmoja ana ubora wake.

 

  1. Lionel Messi

Basi bwana wa kwanza kabisa tunakusogezea mwamba huyu ambae kwasasa anachezea timu yake ya taifa ya Argentina na team ya PSG  ambapo anakadiliwa kuwa na zaidi ya mabao 769. Nyota huyo wa Argentina alifikisha miaka 35 mwezi Juni, licha ya kuwa mkongwe lakini hajapoteza uwezo wake wa kutikisa nyavu na uhodari wake uwanjani.

Mwamba huyo anakubalika na mashabiki wengi kulingana na mafanikio yake ya kubeba viatu vya dhahabu na tuzo mbalimbali mfululizo za mchezaji bora wa mpira wa miguu.
 

  1. Robert Lewandowski

 

Namba mbili bwana inaenda kwa mwamba huyu ambaye anacheza katika timu mbili, moja ikiwa ni timu yake ya taifa ya Poland na nyingine ikiwa ni Barcelona FC ambapo anakadiliwa kuwa na zaidi ya mabao 564. Lewandowski alimaliza ushirika wake wa miaka minane na wababe wa Ujerumani Bayern Munich mapema mwezi huu na kuhamia Uhispania kujiunga na Barcelona.

Lewandowski ni mzuri katika kutumia miguu yake yote miwili katika kutikisa nyavu pale tu anapokutana na wapinzani wake. Mwamba huyu wa Kipoland anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi ulimwenguni. Pia alishinda tuzo za heshima, mataji mawili mfululizo ya bundesliga.

  1. Kylian Mbappe


Mbappe ni mwanasoka rasmi duniani ambae ana uwezo wa kukimbia kasi ya 38km kwa lisaa. Mwamba huyo ambaye ni mchezaji wa timu yake ya taifa ya Ufaransa na klabu yake ya PSG.

PSG wanamuamini Mbappe katika kukimbia na mpira kutoka katikati ya uwanja na kupata magoli mara kwa mara. Mfaransa huyo alimaliza msimu akiwa na mabao 39 katika mechi 46 alizoichezea msimu uliopita na atakuwa mmoja wa kutegemewa wakati Ufaransa itakapoanza kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia mwezi Novemba.

  1. Cristiano Ronaldo


Ronaldo ni mwamba ambaye bado anasalia kuwa mmoja wa vipenzi vya mashabiki akiwa yupo anachezea klabu yake ya mashetani wekundu Manchester United na timu yake ya taifa ya Ureno. Mpaka sasa anahesabiwa kuwa na zaidi ya mabao 815. Winga huyo kama tunavyojua kuwa hakuna taji lolote ambalo Ronaldo ameshindwa kushinda katika kipindi chote cha maisha yake mashuhuri katika mchezo wa mpira wa miguu.

Ronaldo alimaliza msimu uliopita akiwa na mabao 24 akiwa na Manchester United na alikuwa mmoja wa wafungaji bora wa Premier League.

  1. Kevin de Bruyne


Mchezaji huyo wa Manchester City na Ubelgiji anachukuliwa kuwa mmoja wa viungo bora zaidi, mpaka sasa anatajwa kuwa na mabao zaidi ya 157. Sifa nyingi kwa maendeleo yake zinapaswa kwenda kwa meneja wa klabu yake ya sasa Pep Guardiola, ambaye amekuza uwezo wake wa ubunifu.

De Bruyne amebakiza mechi 9 tu kabla ya kuchezea taifa lake akiwa na wachezaji watatu na amefunga mabao 24 akiwa na Die Roten Teufel.
 

  1. Mohamed Salah


Mwamba huyu hapa ana balaa huyo, ana hatari huyoo, sio pouwa. Bwana bwana tuache uongo, Salah wa kimataifa wa Misri bado ni mchezaji mwingine ambaye amefaidika kutokana na kuwa na meneja mzuri wa klabu anayesimamia maendeleo yake. Kijana huyo ambae mchezaji wa timu ya taifa ya Egypt na klabu ya Liverpool anaupiga mwingi na kutajwa kuwa na mabao zaidi ya 280.

Salah amekuwa muhimu kwa mafanikio ya Liverpool katika miaka ya hivi karibuni, ingawa mchango wake kwa Misri haujazaa matunda yoyote hadi sasa. Mpaka muda huu amefunga mabao 156 akiwa na jezi ya Liverpool pamoja na mabao 63 zaidi ambayo amewatengenezea wachezaji wenzake.

 

  1. Karim Benzema


Mmoja wa wasanifu wakuu wa Real Madrid kushinda kombe lao la 14 la Ligi ya mabingwa alikuwa mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema. Mfaransa huyo anachezea katika timu yake ya Ufaransa na klabu ya Real Madrid mpaka sasa ana mabao zaidi ya 441.

Kufuatia kuondoka kwa Ronaldo katika timu Real Madrid, pengo lilikuwa limeonekana kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambayo mshambuliaji huyo mkongwe sasa amefanikiwa kuliziba.

Baada ya miaka sita kutokuwepo kwenye anga ya kimataifa, Benzema amerejea kwenye eneo la nchi yake ya Ufaransa na kurejesha uchawi wake uliosahaulika.

 

  1. Harry Kane

 

Kane ni nahodha (captain) mkuu katika timu yake ya taifa ya England na kuchezea klabu ya Tottenham ambapo kwasasa anatajwa kuwa na zaidi ya mabao 229.

Kama wengine wengi kwenye orodha hii, Kane pia anakuja na uwepo wa angani wa kufunga magori bora zaidi.  Hata kwa Uingereza, uwepo wa Kane akiwa na kitambaa cha unahodha hauwahakikishii tu wachezaji wenzake bali pia mashabiki.

 

  1. Erling Haaland


Hahaha! Nicheke kwanza, huyu nimwamba ambae amewaliza mashetani wekundu (Manchester United) hivi karibuni. Kijana mdogo kabisa ambae amekuwa pasua kichwa kwa timu nyingine pinzani anazidi kupanda katika chat ya kuwa na mabao mengi na kuonyesha ubora wake.

Timu ya taifa ya Norway bado ni jina lisilojulikana katika ulimwengu wa kandanda ya kimataifa. Lakini mchezaji mmoja kutoka nchi ambayo inaikabili dunia kwa dhoruba ni mshambuliaji wao wa futi 6 na inchi 5 Erling Haaland.

Haaland ambae ni mwamba anachezea katika klabu ya Manchester City anakadiriwa kuwa na mabao zaidi ya 200 mpaka sasa, ambapo anaonyesha umahiri wake katika uchezaji wake ambao ndio unamfanya aweze kuwa bora na kuifanya timu yake kushinda katika kila mechi wanayokwenda kucheza nayo.

  1. Neymar


Mwisho kabisa ni Mbrazil huyo ambaye ameona vipaji vyake vingi vikipotea kutokana na matatizo mengi ya majeraha ambayo amekuwa akikabiliana nayo katika kipindi chote cha maisha yake ya soka. Pamoja na hayo, Neymar amebaki kuwa miongoni mwa majina maarufu katika ulimwengu wa soka. Nchi yake inategemea sana uwezo wake wa mpira.

Neymar anatajwa kuwa na mabao zaidi ya 416 na kwasasa anachezea timu yake ya taifa ya Brazil na pia anacheza katika klabu ya PSG ambapo aliamua rasmi kujiunga pamoja mchezaji mwenzie nguli Messi.

Yeye sio mfungaji wa mabao tu bali anayatengeneza pia. Ustadi wake wa kucheza chenga ni kitu ambacho wachezaji wengi wangejivunia. Ingawa hali yake ya sasa katika klabu yake ya PSG ni dhaifu, hakuna kutilia shaka uwezo wake.

Soka la mpira wa miguu  linazidi kuwa na ushindani kila kukicha na hakuna uhakika kwamba mchezaji mmoja anachukuliwa kuwa mchezaji bora wa kandanda duniani kwa sasa aitakuwa hivyo kwasababu kila mmoja ni bora zaidi.

Oyaaaweeeh! Haya embu njoo katika mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop na udondoshe komenti yako kwa kutujuza ni nani kwa mtazamo wako wewe ni nani mchezaji bora wa soka duniani?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags