Waathirika wa ajali ya Precision Air kulipwa fidia kwa siri

Waathirika wa ajali ya Precision Air kulipwa fidia kwa siri

Mkurugenzi wa Shirika la Precision Air, Patrick Mwanri, amesema mchakato wa malipo utakuwa kati ya familia za waliothirikana ajali ya ndege na utafanyika kwa umakini mkubwa.
 
Mwanri amesema, “Shirika letu lina bima na ipo kulingana na taratibu za uendeshaji mashirika ya ndege. Taratibu zimeshaanza na wahusika tumeshaanza kuwasiliana nao ili waweze kupata taarifa rasmi ya nini kinahitajika,"
 
Ndege ya Precision Air ilianguka Ziwa Victoria takribani mita 100 kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikiwa na watu 43 ambapo 19 kati yao walifariki dunia wakiwemo marubani wawili.
 
 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags