Hapa sijui kama nicheke au nisikitishe maana mambo ni mambo muraaa!!
Sidhani kama kuna siku tulitegemea kuona wananchi kushikwa na hasira hadi kuamua kuvamia nyumba ya Rais wao na kumtimua mbiooo afu wakaanza kujistarehesha humo.
Inashangaza lakini hayo ndiyo tunayoyashuhudia huko Sri Lanka ambapo wananchi WAMECHOKAAAAA!
Baada ya balaa hilo kuanza, wananchi wakaamua kuvamia nyumba ya Rais wao iliyosheheni starehe za kila aina na kuitumia nyumba hiyo kama nyumbani kwao.
Wapenda mbwa, wakabeba wao.
Wapenda wasiowahi ingia conference room nao wakafurahia conference room ya Rais.
Wale ambao walikuwa hawana pa kulala, nao wakapata pa kujishikiza.
Kweli kisa hiki kimekuwa na vituko vya kila aina, yote haya, wananchi wametaka Rais na Waziri wake Mkuu kujiuzulu.
Lakini, licha ya Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ranil Wickremesinghe kukubali kujiuzulu, waandamanaji wamesema hawataondoka na wataendelea kubaki kwenye makazi ya viongozi hao mpaka watakapoachia ngazi rasmi.
Spika wa Bunge la nchi hiyo alitoa taarifa kuwa Rais Rajapaksa amekubali kujiuzulu na atafanya hivyo rasmi Julai 13 lakini tangu tangazo hilo litolewe Jumamosi Julai 9, 2022, Rais mwenyewe hajaonekana wala kutoa taarifa kwa umma.
Waziri Mkuu naye alisema atajiuzulu kutokana na maandamano ya Jumamosi, ambapo makazi yake binafsi yalichomwa moto.
Pamoja na kutangaza kuachia ngazi, lakini waandamanaji wameendelea kusalia kwenye makazi ya viongozi hao na baadhi wakiingia kwenye ndani ya nyumba ya Rais na ‘kujiachia’.
Leave a Reply