Vitu vya kuanzisha ukiwa chuoni

Vitu vya kuanzisha ukiwa chuoni

Hellow! Wanangu wa vyuoni hatujawahi angushana hata siku moja na kama kawaida yetu katika segment ya UniCorner tunakusogezea mada konki kabisa. Tunajua week kadhaa mbeleni basi wanachuo wote wanakuwa wamerudi kwa ajili ya kuendelea na masomo na wengine ndo kwanza wanaanza first yeah.

Sasa leo tumekusogezea mada ambayo itakujuza kuhusiana na vitu vya kuanzisha ukiwa chuoni, mambo yenyewe yakiwa ni

  • Biashara
  • YouTube channel
  • Blog
  • Kujenga mahusiano na wale watu wanaofanya vitu vinavyo endana na wewe

Hakuna wakati mzuri wa kujiandaa na maisha ya kitaa/mtaani kama ukiwa chuo, niwape tu siri. Mkifika huku mtaani halafu hauna plan, unaweza pata hadi depression kwa jinsi life litakavyokushtua.

YOUTUBE CHANNEL

Unaweza anzisha YouTube channel ukaikuza ukiwa chuo kwa kushare video mbalimbali hata za palepale chuoni. Najua utajiuliza kwanini nasema hivi lakini kabla hujaanzisha tafuta mtu mwenye utaalamu na mambo hayo akujuze vizuri ndo utaelewa nini namaanisha.

Hata ukiangalia sasa hivi vijana wengi wamejikita katika kuanzisha channel zao na kujipatia kipato kupitia content zako za video.

 

FUNGUA BLOG

Unaweza anzisha blogu ukashea ujuzi na hivyo kujimarket vizuri mtaani na ukajipatia pesa kupitia matangazo. Wafanyabiashara wengi wakubwa hutangaza biashara zao kupitia blog za watu tofauti tofauti, so ukiwa unaandika content nzuri katika blog yako itakufanya ujulikane na kukupatia kipato pia.

ANZISHA BIASHARA

Pia unaweza anzisha biashara unayoweza kuiendesha hata ukimaliza kama sio tu kuwa chanzo cha msingi cha kukusapoti chuoni.

JENGA MAHUSIANO NA WATU

Mwisho kabisa unaweza wafuatilia wale wanaofanya mishe unazopenda, study the greatest, uwe the greatest tu. Watafute wakikujibu sawa, wasipokujibu sawa, jitahidi kufanya hata part time ya kujitolea sehemu kwa wikiendi kwa ajili ya tengeneza connection.

Ukiweza kufuatisha mambo haya, basi utajikuta hadi pale unapoenda kugraduate, una experience nzuri na yakutosha na ushajenga uzoefu wa kitu ulichoamua kufanya, hivyo kuongeza chances zako za kutoboa mtaani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags