Urafiki chuoni uko hivi

Urafiki chuoni uko hivi

Wanangu wa chuoni mambo vipi. I hope mko pouwa kabisa, sasa leo katika segment yetu ya UniCorner tunakusogezea elimu ambayo hutaipata kwa mtu yoyote bali Mwananchi Scoop tu, sisi huwa hatutaki kukuficha jambo lolote lile ambalo linaweza kwako kuwa baya ama zuri.

Siku zote bwana urafiki unatokea tu kwa kukaa kwa muda mrefu pamoja au kuendana yaani na maanisha kuna kitu kinawasukuma tuu kuwa marafiki.

Sasa basi chuoni unaenda kukutana na watu wapya. Okay sio wote, kuna wale uliokuwa nao secondary or primary lakini asilimia kubwa watakuwa wapya kwako yaani hamjuani kabisa ndo kwanza kuwaona katika maisha yako.

That is exciting and scary at the same time. Watu wapya utakaoanza na moja kuwafahamu, utaanza upya kuwa karibu nao, utaanza kuishi nao maisha na watakuwa kwenye memory yako milele na kila ukikumbuka chuo utakuwa unamkumbuka kwa jema alilokutendea au baya.

Urafiki chuoni wakati naenda chuo kuna mtu aliniambia kuwa watu unaokutana nao chuo unaweza dumu nao muda mrefu kwenye maisha, kwasababu mmekutana nao kipindi uko kwenye the most defining time of your life lakini pia kama vile mambo mengine kwenye maisha yalivyo na mwanzo na mwisho sometimes pia urafiki unaisha.

Chuoni kuna urafiki wa aina tatu nao ni:

  • Urafiki kutokana na kwamba mpo sehemu moja mfano mpo course moja, group moja la assignment, room moja hostel nk
  • Urafiki kutokana na kwamba mnapenda vitu sawa ie, mnakutana club kwahiyo mnashtuana kwenda, mnasali pamoja, mnacheza sports
  • Urafiki kutokana na kwamba mmeamua kuwa marafiki na kuwa there for each other aim for the last one, because that one will last.

Nilikuwa na marafiki wengi chuo, waliodumu ni wale nilikuwa nimeweka uamuzi kua nataka wawe kwenye maisha yangu, we all need people around us. Marafiki ni familia unayoichagua wewe mwenyewe awe mbaya au mzuri.

Chagua wisely, acha moyo wako uchague rafiki unaemtaka na kumpenda. Amua watu unaotaka wadumu na invest in that friendship. Invest in it.

Amua watu unaotaka wakae kwenye maisha yako and let them know that is what you want. It is important if they feel the same way, ili urafiki usiwe wa upande wako pekee.

Naamini utapata marafiki wapya, wachague wale unaoona wanaelekea kule unatamani maisha yako yaelekee.
Ukimaliza chuo, you can look back and see that you don’t have regrets. Now that unaenda, you have a chance to build a regret free life.
Who are you choosing?

Kingine nachotaka kukwambia ni kuhusiana na kuna baadhi ya watu watakupenda ukiwa chuo watataka urafiki na wewe kwasababu tu unakitu fulani mkishamaliza chuo basi huwaoni kabisa, chagua mtu ambaye hata mkimaliza chuo basi mtakuwa pamoja siku zote. Kaulimbiu yetu sasa ni hatuchagui marafiki mboga.

I hope tunaelewana katika hili nakusisitizia kabisa, chagua marafiki ambao unaendana na wewe sio crush crush lakini ucrush wenu wa kukutana klabuni tu na sio wa maendeleo, kwa mada konki kama hizi usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags