Ooooooh! Kama kawaida yetu tunazidi kukusogeza gurudumu katika kukufanya wewe mfuatiliaji wetu upate kitu moyo unapenda. Sasa leo katika segment yetu ya afya tunakusogezea mada ambayo watu wengi wakiona wana matatizo hayo wanachukulia ni kawaida lakini sisi tunakujuza ili uweze kupata matibabu haraka iwezekanavyo.
Kuvimba fizi kitaalamu ‘gingivitis’ ni changamoto ya meno inayotokea kila mara na mara chache sana huleta tatizo kama isipotibiwa haraka. Dalili za kuvimba fizi ni pamoja na fizi kututumuka na kuwa nyekundu sana.
Changamoto ya fizi kuvimba mara nyingi huisha yenyewe kwa kuzingatia tu usafi wa kinywa, kama kupiga mswaki mara mbili kwa siku na kila baada ya Kula chakula. NB:Kwa nyongeza unaweza kufanya ‘coconut oil pulling’ kusafisha meno badala ya kutumia mouthwash ambazo zina madhara.
AINA ZA TATIZO LA KUVIMBA FIZI
Kuna aina kuu mbili za tatizo la kuvimba fizi.
- Dental paque-induced gingival disease; Husababishwa na utando kwenye jino, matumizi ya baadhi ya dawa na ukosefu wa lishe bora
- Non-plaques induced gingival lesions; Husababishwa na aina fulani ya bakteria, virusi au fangasi. Pia yaweza kusababishwa na changamoto za kurithi, vidonda na aleji ya vitu vya nje.
NINI KINASABABISHA KUVIMBA FIZI
- Chanzo kikuu cha kuvimba fizi ni utando wenye mrundikano wa bakteria katikati ya meno.
Utando huu unapelekea kinga ya mwili kupambana na bakteria na hivo kupelekea tishu za karibu kuumia na kuvimba. Pia inaweza kupelekea tatizo kubwa la kuoza jino kabisa endapo hutapata tiba mapema.
Utando wa kwenye jino hufanyika ili kulinda jino lisishambuliwe na vimelea wabaya. Lakini utando huu usipoondolewa mapema kwa kupiga mswaki, unageuka kuwa nta chini ya jino na kwenye fizi. Nta hii huwa na rangi ya njano na hupelekea fizi kuvimba.
- Vyanzo vingine vya fizi kuvimba. Mabadiliko ya homoni:
Hii inaweza kutokea wakati wa kubalehe, kukoma kwa hedhi-menopause, kwenye mzunguko wa hedhi na wakati wa ujauzito.
- Baadhi ya magonjwa:
Kama saratani, kisukari, HIV hupelekea fizi kuvimba
- Dawa:
Afya ya kinywa inaweza kuathiriwa na matumizi ya baadhi ya dawa, hasa zile zinazopunguza kiwango cha mate mdomoni.
- Kuvuta sigara:
Wavutaji wa sigara wapo kwenye hatari zaidi ya kuvimba fizi ukilinganisha na wale wasiovuta sigara
- Umri:
Hatari ya kuvimba fizi inaongezeka zaidi kadri unavyozeeka
- Lishe mbovu:
Upungufu wa vitamin C kwenye lishe yako hupelekea magonjwa ya fizi.
- Historia ya kuugua kwenye familia:
Kwa wale ambao wazazi wao wana matatizo ya fizi, wako kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo.
DALILI YA FIZI KUVIMBA
Kwa tatizo ambalo ni dogo, unaweza usipate shida yoyote na pengine usigundue kabisa kama fizi zimevimba. Kwa tatizo kubwa unaweza kupata dalili hizi:
- Fizi kuwa nyekundu sana
- Kulainika kwa fizi na kuuma
- Kutokwa damu kwenye fizi wakati wa kuswaki
- Harufu mbaya mdomoni
- Vipimo kugundua tatizo
- Mtaalamu wa magonjwa ya meno (dentist) atakuchunguza uwepo wa nta na utando na kukuuliza dalili unazopata
MATIBABU YA KUVIMBA FIZI
Tiba kwa changamoto ya kuvimba fizi inahusisha huduma kutoka kwa mtaalamu wa meno, usafi wa meno ukiwa nyumbani na pia kuendelea kuhudhuria kliniki ya meno.
HUDUMA YA NYUMBANI
Kulinda afya ya meno yako tunashauri:
Kusafisha meno mara mbili kwa siku, asubuhi na usiku kabla ya kulala.
Tumia uzi wa kusafisha uchafu katikati ya meno.
Baada ya kula suuza mdomo na maji na uteme.
Tumia coconut oil pulling kusafisha meno.
Ni matumaini yangu kwa maelezo hayo madogo yameweza kukupatia ufafanuzi ni jinsi gani utaweza kutatua tatizo hili. Madaktari wengi wanashauri kutopuuza ugonjwa wowote hata kama ni mdogo maana ukiwa mkubwa utakuletea matatizo makubwa zaidi.
Imeandaliwa na Mark Lewis
Leave a Reply