Hali ya chango au tumbo kuunguruma wakati wa hedhi inaweza kumfanya mwanamke akakosa raha kabisa. Mwanamke anaweza kujihisi kama vile mwili wake umeongezeka uzito au kwamba tumbo lake limejaa na kuanza kupumua. Lakini pia, huwa kuna mabadiliko ambayo mwanamke anaweza kuyapata na kupunguza dalili hizo.
Tumbo linapokuwa likiunguruma au chango ndio wakati mwanamke anapoanza kuhisi tumbo lake kuwa limejaa tena zito kabla au pindi anapoingia hedhini.
Baadhi ya wanawake wamekuwa wakisumbuliwa sana na maumivu chini ya tumbo au usawa wa kitovu. Na mara nyingi maumivu haya huwapata wasichana waliokwisha vunja ungo na wanawake watu wazima wenye umri wa kuzaa.
Chango la uzazi ni miongoni mwa magonjwa yanayoshambulia viungo vya uzazi vya mwanamke ambapo humsababishia maumivu makali ya tumbo na kushindwa kupata ujauzito, au mimba kuharibika kila zinapoingia.
CHANGO HUSABABISHWA NA NINI
Matatizo ya chango la uzazi, inatokana na vifuko vya mayai ya uzazi (ovaries) kutokuwa na uwezo wa kuzalisha mayai na kufanya yakue kwa wakati muafaka.
Mwanamke mwenye matatizo haya hushindwa kuwa na siku za hatari za kunasa ujauzito na kama zipo basi huwa hazina mpangilio unaoeleweka.
Pia chango inaweza kutokana mabadiliko ya kiwango cha vichochezi au homoni za progesterone na estrogen.
Viwango vya homoni ya progesterone hushuka karibia wiki moja kabla kipindi cha hedhi cha mwanamke hakijaanza.
Kupungua kwa kiwango cha homoni hii husababisha ngozi laini ya ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus) kubanduka, hali ambayo ndiyo husababisha kuvuja kwa damu ya hedhi.
DALILI ZA CHANGO LA UZAZI.
Dalili za chango la uzazi kwa mwanamke ni pamoja na:
- Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi
- Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
- Hujisikia homa kali anapokaribia siku zake za hedhi
- Kujisikia uchovu mkubwa anapokaribia siku zake za hedhi.
- Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi ambapo mwanamke anaweza kuwa na mzunguko wa hedhi wa takriban siku 35.
- Kubadilikabadilika kwa siku za hedhi.
- Kuwa na mzunguko mfupi wa hedhi chini ya siku 21.
- Kuwa na hasira kali anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi.
- Kupata michubuko sehemu zake za uke.
- Kuchukia kushiriki tendo la ndoa
- Kupata uvimbe kwenye kizazi.
- Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi.
MADHARA YA CHANGO LA UZAZI KWA MWANAMKE.
Na ufahamu kuwa, tatizo la chango lisipotibiwa mapema likapona linaweza kusababisha madhara haya yafuatayo;
- Mwanamke anaweza kuwa mgumba kabisa
- Kuwa na uke mdogo sana
- Vigumu kupata ujauzito na hata pale anaponasa ujauzito, huharibika kwa mimba na kutoka kwa mimba
- Kushindwa kufurahia tendo la ndoa ambapo huwa vigumu sana kwa mwanamke mwenye tatizo hili kufika kileleni wakati wa tendo.
NB:- Chukua tahadhari mapema Kwa kufika katika kituo cha afya, au kumwona mtaalamu wa afya kutatua tatizo hili. Kinga ni Bora kuliko tiba.
Leave a Reply