Tyla, Ayra hawashikiki Spotify

Tyla, Ayra hawashikiki Spotify

Zikiwa zimepita siku chache tangu albumu ya mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Tyla kufikisha zaidi ya wasikilizaji (streams) bilioni moja katika mtandao wa Spotify na sasa ni zamu ya Ayra ambaye ametajwa kuwa msanii aliyesikilizwa zaidi kwa mtandao huo kwa mwezi.

Msanii huyo kutoka Nigeria ametajwa kumpiku Tyla kwa kuwa na wasikilizaji wa mwezi milioni 31.4 huku Tyla akiwa na wasikilizaji milioni 31.2 kwa mwezi uliopita.

Tyla na Ayra ni moja ya wasanii wa kike kutoka Afrika ambao wanaongoza kuwa na namba kubwa zaidi za wasikilizaji kwenye mtandao wa ‘Spotify’. Ambapo kwenye mtandao huo mwanamuziki Rihanna ndiye anaongoza kuwa na wasikilizaji milioni 84.9.

Wakifuatia SZA milioni 74.1, Beyonce milioni 62.7, Doja Cat milioni 56.1, Nick Minaji milioni 47.9, Cardi B milioni 31.7, Raye milioni 31.6, Ayra Starr milioni 31.4, Tyla milioni 31.2 huku nafasi ya 10 ikikamatwa na Summer Walker akiwa na wasikilizaji milioni 28.3.

Kwa upande wa wasanii wa kike kutoka Bongo ambao wanawasikilizaji wengi kupitia mtandao wa huo ni Zuchu ambaye anaongoza kwa kuwa na streams zaidi ya laki mbili na elfu tisini na sita.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post