Tyla aipiku rekodi ya Burna Boy

Tyla aipiku rekodi ya Burna Boy

Nyota wa muziki kutoka nchini Afrika Kusini ameripotiwa kuwa ndiye msanii anayefanya vizuri Barani Africa baada ya kupata waskilizaji wengi kupitia mtandao wa Spotify huku akiipiku rekodi ya Burna Boy.

Tyla ameipiku rekodi hiyo ya mkali wa Afrobeat Burna kwa kupata zaidi ya wasikilizaji milioni 630 ndani ya wiki moja kupitia albumu yake mpya iitwayo ‘Tyla’.

Albumu hiyo yenye ngoma 14 iliachiwa rasmi Machi 22, mwaka huu huku baadhi ya ma-staa kutoka Marekani wakishilikishwa akiwemo Travis Scott, Kelvin Momo na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags