TWALHAT KIONE: Mhitimu alieamua kuwa mtengenezaji wa picha mbao na graphics designing

TWALHAT KIONE: Mhitimu alieamua kuwa mtengenezaji wa picha mbao na graphics designing

Hellow! Nyie nyie mwezi huu si wawanawake bwana nimeamua kuwasogezea mabinti ambao wanajituma wanachakarika kiufupi tunaweza waita ‘super woman’ chipukizi.

Leo na mwezi huu wote kwenye segmnenti yetu ya unicorner tunakuja kukuelimisha wewe muhitimu ambaye bado haujafanikiwa kupata ajira usikubali kubaki tuu nyumbani kwasababu hauna cha kufanya wakati wenzako wengine huku wanajitoa ili watimize ndoto zao.

Week iliopita bwana tulikuwa nabinti ambaye alieibua hisia za watu wengi kutokana ka komenti tulizo pata katika stori yake ya kuwasaidia mabinti wengine wasipitie walichokipitia huyu Madam hedhi salama Shufaa Nassor.

Sasa leo bwana nakuzogeza binti mwingine ambaye ameamua kuchukuwa coz ambayo mabinti wengi wanaikimbia kutokana na ugumu wake lakini kwa upande wake alipamabana nayo na ndo anayo amini kuwa itamuendeshea maisha yake yotee.

Twalhat Ibrahim Kione ambaye ni mwanafunzi aliehitimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam course ya ‘Bachelor of arts in art and design, katika department ya creative art.

Binti huyu  kupitia timu yetu ya Mwananchi Scoop tuliweza kupiga stori nae kuhusu maisha yake baada ya kumaliza chuo, changamoto anazokumbana nazo na vipi kupeleka CV katika kampuni yoyote ile, so ungana nami kujua Zaidi…

Kwasasa binti huyu yeye hakuamua kukiweka kando kipaji chake na kuendelea na kujishughulisha na maswala ya graphics designing and art kama painting drawing, na uuzaji picha mbao ambapo ni biashara ilioshamiri sana nchini. Ndio hiyo inayomsaidia kujikimu kimaisha japo si sana lakini kinamsaidia kwa aina yake.

Alipata nafasi ya kujiendeleza na kutengeza connection tofauti tofauti kutokana na kuchanganyika na watu wa carrier yake ili kujifunza na kuweza kupata ujuzi wa kazi anazozifanya (graphics designing). Licha ya hio aliamua kujifunza maswala yanayohusiana na printing na jinsi ya kutengeneza masoko kulingana na biashara ya graphics.

Mwanadada huyo aliamua kufunguka kuhusiana na upataji wake wa kazi ambapo ndo sehemu anayojishikiza kwasasa na kusema kuwa..

 “Alhamdullah nilipata bahati ya kupata nafasi ya kujitolea kazi as soon nilivyomaliza chuo kwasababu nilijitengenezea uzoefu kwa kipindi ambacho niko chuoni,  hivo haikua inasumbua sana kwenye swala Zima la kupata kazi na pia kuwa na watu wenye moyo wa kujitoa wameniwezesha kunifanikisha hapa nilipo” amesema Twalhat Kione

Siku zote changamoto ndio jambo ambalo linamkwamisha sana mwanadamu kufanya mipango na kutimiza malengo yake kwa upande Twalhat yeye changamoto anazokumbana nazo ni..

“Changamoto kubwa ninayo kumbana nayo  ni muda wa kupata kwaajili ya kujifunza na kukutana na watu in person especially in issues of printing na pia utayari wa watu kukufundisha kwasababu ya personal issue zao so either wanakupa some of it or wanakupiga calenders amesema Binti huyo.”

Kila mtu kuna ule msoto anaoupitia wa kutembea na jua kali kwasababu ya kutembeza CV katika makampuni mbalimbali, kwa upande wa binti huyu bwana yeye alieleza kuwa…

“Nilishawahi fanya interview na kutuma CV baadhi ya maeneo na sehemu nyingine walisema wataniita and hawakuniita so nikawaida kwasababu kila company ina quality zao na hawawez chukua kila mtu cha muhimu kwangu ni kumshukuru mungu co mabaya naweza kujikimu kwenye shida ndogo ndogo kama maswala ya nauli mavavi Kodi na vitu vidogo vidogo” amesema Twalhat Kione

Cha muhimu kuzingatia ni kuhusiana na kutokukata tamaa hata siku moja najua wengi wenu mmeshazunguka sana na CV zenu kupeleka katika makampuni mbalimbali lakini lakini hakuna alichoambulia, so usikate tamaa labda sehemu uliokwenda sio rizki yako usibweteke chakarika ili uweze kutimiza ndoto zako.






Comments 2


  • Awesome Image
    Nilham kione

    She is my sister my heroin mpambanaji may Allah bless u ñ reach unapotak always my roll model very inspiring😍😙

  • Awesome Image
    Nilham kione

    She is my sister my heroin mpambanaji may Allah bless u ñ reach unapotak always my roll model very inspiring😍😙

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags