Trump kufunguliwa akaunti yake ya Facebook na Instagram

Trump kufunguliwa akaunti yake ya Facebook na Instagram

Aliekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump ataruhusiwa kurudi kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram, baada ya Meta kutangaza kumfungulia akaunti zake.

Akaunti zake zitafunguliwa "katika wiki zijazo", kampuni kubwa ya mitandao ya kijamii ilisema.

Katika taarifa yake, Nick Clegg, rais wa masuala ya kimataifa wa Meta, aliuambia umma kuwa  "unapaswa kusikia kile wanasiasa wao wanasema".

Trump alizuiwa kutumia Facebook na Instagram baada ya ghasia zilizotokea Capitol mnamo mwaka 2021.

"Kampuni hiyo ilichukua hatua hiyo baada ya Trump kujisifu kuhusika katika ghasia katika ikulu ya Capitol", Clegg alisema.

"Maamuzi ya kumfungia mitandao yake ya kijamii yalikuwa ya ajabu kutokana na mazingira," aliongeza.

Alisema uchunguzi umebaini kuwa akaunti za Trump haziwakilishi tena hatari kubwa ya usalama wa umma. Lakini kwa sababu ya "ukiukaji" wa zamani sasa atakabiliwa na adhabu kali kama makosa yakijirudia.

Aidha Republican wamekuwa wakishinikiza Trump aruhusiwe kurejea kwenye mtandao wa FaceBook anapojitayarisha kuwania urais tena mwaka ujao.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags