Tems, Rema, Tyla kwenye Playlist ya Obama

Tems, Rema, Tyla kwenye Playlist ya Obama

Kama ilivyo desturi kwa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama kila ifikapo katikati na mwisho wa mwaka kuachia Listi ya ngoma anazopenda kuzisikiliza, hatimaye usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2024 Obama ameshusha orodha ya nyimbo anazozikubali.

Kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter) Obama ame-share listi ya ngoma hizo ambazo anazisikiliza zaidi katika kipindi hichi cha kiangazi (Summer Playlist) huku akitumaini kuwa watu wanaomfuatilia watapata kitu cha kusikiliza.

“Wakati majira ya joto yakikaribia kuisha, nilitaka kushiriki baadhi ya nyimbo ambazo nimekuwa nikisikiliza hivi karibuni na isingekuwa orodha yangu ya nyimbo kama haingekuwa na mchanganyiko wa aina mbalimbali, Natumaini utapata kitu kipya cha kusikiliza” ameandika Obama

Wasanii ambao wamefanikiwa kuingia katika Playlist hiyo ya Obama ni pamoja na Tems, 2Pac, Rema, Tyla, Beyoncé, Billie Eilish, Bob Marley na wengineo.

Hata hivyo kufuatia na listi yake hiyo Obama ameonekana kuvutiwa zaidi na ngoma za marehemu ‘Rapa’ Tupac ambapo kupita Summer Playlist ya mwaka 2023 kulikuwepo na wimbo wa msanii huyo uitwao ‘California Love’ aliomshirikisha Dr. Dre na Roger vile vile katika listi yake ya mwaka huu upo wimbo wa msanii huyo uitwao ‘How do you want it’.
Imeandikwa na Aisha Lungato






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags