Taylor Swift akataa kulipwa tsh 23 bilioni

Taylor Swift akataa kulipwa tsh 23 bilioni

‘Rapa’ kutoka nchini Morocco French Montana amedai kuwa mwanamuziki na bilionea Taylor Swift alikataa kufanya show katika sherehe binafsi za Falme za Kiarabu ambapo aliahidiwa kulipwa dola 9 milioni sawa na tsh 23 bilioni.

Montana ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahijiano na #VladTV ambapo ameeleza kuwa mwezi Disemba mwaka jana alipokea ofa kwa ajili yake na Swift ili waweze kutumbuiza pamoja kwenye moja ya sherehe huko Uarabuni ambapo yeye alitakiwa kulipwa dola 1 milioni, lakini mwanamuziki huyo kutoka Marekani aliikataa ofa hiyo.

Aidha mpaka kufikia sasa bado haijafahamika sababu za Swift kukataa dau kubwa kama hilo, ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu #TaylorSwift aliingia kwenye orodha matajiri wakubwa duniani.

Ambapo ametajwa kumiliki utajiri binafsi wastani wa dola 1.1 bilioni ikiwa ni sawa Sh 2.5 trilioni huku idadi hiyo ya fedha ikimfanya kuwa mtu wa 2,545 kati ya 2,781 ya mabilionea wa mwaka 2024.
.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags