Somo la kuchinja na kupika kuku lazua mjadala nchini Kenya

Somo la kuchinja na kupika kuku lazua mjadala nchini Kenya

Picha ya video inayoonyesha watoto wawili wa shule ya msingi wakichinja kuku nchini Kenya imezua mijadala kuhusu mtaala mpya wa nchi hiyo unaozingatia zaidi ujuzi wa vitendo - Competency Based Curriculum (CBC).

Wanafunzi wa shule ya msingi wamekuwa wakitumika kufanyiwa utafiti kwa ajili ya mtaala mpya na wamepitia mazoezi mbalimbali ya vitendo kwa kipindi cha miaka michache iliyopita kuanzia kutengeneza sanamu za kuwatisha ndege wanaoharibu mimea hadi kuuza bidhaa kwenye masoko.

Wanaounga mkono mtaala wenye msingi wa ujuzi - Competency Based Curriculum (CBC) wanasema ni uboreshaji wa nadharia za zamani na mfumo wenye msingi wa mtihani kwani unawaandaa zaidi kwa ajili ya maisha na kupata ajira katika karne ya 21.

Pia walidai kuwa kwasababu kuna tathmini inayoendelea itapunguza udanganyifu katika mitihani, ambao limekuwa ni tatizo kubwa kwa serikali.  

Takriban wanafunzi milioni 1.25 wa darasa la sita watafanya mtihani hivi karibuni kama sehemu ya  kupata cheti cha kumaliza shule ya msingi ambacho kinatoa fursa ya mwanafunzi kujiunga na shule ya sekondari.   

Kwa mara ya kwanza, mtihani utachangia 40% ya maksi za mtihani wao wa mwisho kwani alama za mitihani ya tathmini waliyoifanya tangu darasa la kwanza itachangia 60% zilizosalia.

Lakini baadhi ya wazazi hawafurahishwi na gharama ya mtaala mpya kwani shule huwategemea kuchangia zana na fedha kwa ajili ya vitu  kama – kuku – wanaohitajika kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.

Mwalimu wa sayansi kimu katika Shule ya Msingi ya Kangundo, mashariki mwa Kenya anasema wale wanaotoka katika familia zenye kipato cha chini wakati mwingine wanalazimishwa kuwatazama wenzao wakijifunza kwa vitendo.   

 "Wanafunzi wangu wa darasa la tano, kwa mfano, walikuwa wakishona leso kwa ajili ya mradi na baadhi hawakuwa na uwezo wa kununua kitambaa, kwahiyo tuliishia kutumia vichache ambavyo vilinunuliwa na baadhi ya wanafunzi," Jemimah Gitari aliiambia BBC.

Kufuatia somo la vitendo la kuku – lililofanywa na wanafunzi wa darasa la sita kote nchini mwezi Septemba – picha zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zionyesha waalimu wakionekana kula kuku katika ofisi za waalimu. 

Mbunge kutoka magharibi mwa Kenya, Didmus Barasa, aliwashutumu kwa kufanya karamu kwa chakula kilicholipiwa na wazazi ambao hawana uwezo wa kukinunua.

"Sasa hakuna kuku kwenye nyumba za watu," alisema katika kauli iliyokasirisha muungano wa waalimu.

 Mjadala mkali wa kuku hata uliyafikia masikio ya rais mpya wa Kenya Rais William Ruto, ambaye ameweka kamati ya kikosi kazi cha wajumbe 49, kitakachotathmini mtaala mpya, ambao ulikuwa mradi mdogo wa mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta.

Wajumbe wa kamati hiyo wana hadi kufikia mwisho wa mwaka huu kutoa mapendekezo kuhusu iwapo mtaala wa CBC unaweza kuendelea kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la sita kuweza kuendelea katika elimu ya sekondari, ambao wanatarajia kuanza mwezi Januari.    

"Vitabu na mtaala vilivyotayarishwa viko tayari lakini tunasubiri ushauri kabla ya kuvisambaza," Profesa Charles Ong'ondo, ambaye anaongoza  Taasisi ya Kenya ya maendeleo ya mtaala (The Kenya Institute of Curriculum Development) aliiambia BBC.   

Baadhi ya wazazi hawana tatizo na suala la wanafunzi kujifunza kwa vitendo lakini wanasema mtaala unakosa uwiano kwani kazi za vitabuni ni kidogo.

 

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post