Sokwe wa MJ sasa ana miaka 40

Sokwe wa MJ sasa ana miaka 40

Sokwe maarufu wa marehemu mkali wa Pop Michael Jackson, aitwaye Bubbles ameripotiwa kufikisha miaka 40 ambapo kwasasa anatunzwa katika kituo cha kulea wanyama cha Apes Wauchula, Florida nchini Marekani.

Kwa mujibu Wealth Sokwe huyo analipiwa dola 25,000 kwa ajili ya matunzo kila mwaka ambapo fedha hizo zinalipwa na familia ya MJ.

Ikumbukwe kuwa Michael alimnunua Bubbles kutoka katika kituo hicho alipokuwa na umri wa miezi nane ambapo aliuziwa na mkufunzi wa wanyama wa Hollywood kwa dola 65,000.

Michael na Bubbles hawakuwahi hutengana hata mara moja mpaka pale mwanamuziki huyo alipofariki ambapo Sokwe huyo aliishi kwenye nyumba ya familia ya Jackson huko Los Angeles, lakini baada ya muda aliondolewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags