Shamsa Ford hana bahati ya kuhongwa

Shamsa Ford hana bahati ya kuhongwa

Wanasemaga usililie vingine, wewe lilia tu bahati!

Basi bwana katika harakati za maisha za hapa na pale, Star Wa Filamu Bongo 🇹🇿 anayejulikana kama Shamsa Ford amesema kuwa yeye hanaga bahati ya kuhongwa bali huwa anapambana mwenyewe mpaka kieleweke.

Muigizaji huyo alitema nyongo za kutosha katika Refresh ya WasafiTv, ambapo alieleza ni namna gani alivyohangaika na maisha hadi kupitia muda ambao alilala chini na mwanae, Terry.

"Sinaga Bahati Ya Kuhongwa," alisikika Shamsa Ford.


Ikumbukwe tu kuwa Shamsa alishawahi kuolewa na mmiliki wa duka za nguo, Chidi Mapenzi ambapo inasemekana kuwa ndoa yao ilipitia misukosuko mingi hadi ikadondoka chaliiii.



Msanii huyo pia aliwahi kuhusishwa na Ney wa Mitego.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags