ROTIMI:  Kheri kuishi Afrika kuliko Marekani, Kuna Utajiri zaidi, wanaishi vizuri mara 10 ya sisi

ROTIMI: Kheri kuishi Afrika kuliko Marekani, Kuna Utajiri zaidi, wanaishi vizuri mara 10 ya sisi

Muigizaji na msanii wa muziki ambaye pia ni shemela wa taifa, Olurotimi Akinosho "Rotimi" amesema kuwa Africa ni matajiri kuliko hata Marekani na kwamba ni kheri kuishi Africa.

Akiwa katika interview moja hivi karibuni, muimbaji huyo aliyetamba sana na nyimbo ya 'Love Somebody' alisema kuwa, "Watu wengi hawajui tu! Rudini Africa mkatembee, Afrika ni tajiri sana. Marekani kuna utajiri ila Afrika kuna matajiri,"



Rotimi ambae yupo katika penzi zito na msanii kutoka nchini Tanzania, Vanessa Mdee, aliendelea kusisitiza kuwa, "Ukiwa una hela Africa, haijalishi nchi gani, utaishia vizuri mara 10 zaidi kuliko watu wengi matajiri Marekani."

"Kila kitu cha Marekani kimeibiwa kutoka Africa," alisema Rotimi.

Rotimi aliongeza, "Marekani unapumuwa matatizo tu, kule hata hali ya hewa ni nzuri."



Tuambie, would you rather live in Africa or in America?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags