Ronaldo apewa tuzo na Guinness baada ya kucheza mechi 200

Ronaldo apewa tuzo na Guinness baada ya kucheza mechi 200

Cristiano Ronaldo amepokea Rekodi ya Dunia ya Guinness baada ya kuichezea Ureno mechi 200 za kimataifa.

Mshambulizi huyo mashuhuri alicheza mechi yake ya 200 akiwa na ‘Selecao das Quinas’ katika mechi yao ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Iceland na kuvunja rekodi nyingine ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika soka la kimataifa.

Mafanikio ya Cristiano Ronaldo yametambuliwa na Guinness Book of Records, nahodha huyo wa Ureno alikabidhiwa cheti cha mafanikio yake kabla ya pambano la Taifa lake dhidi ya Iceland.

Ni rekodi nyingine ya kuongeza kwenye orodha ndefu ya Ronaldo ya mafanikio katika soka ya kimataifa. Mchezaji huyo wa mbele wa Al Nassr ndiye mfungaji bora wa muda wote katika soka ya kimataifa akiwa na mabao 122 katika michezo 200 hadi sasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags